Kumekuwa na ghasia zaidi katika mgodi wa
Marikana nchini Afrika Kusini.
Helkopta ya jeshi la polisi nchini Afrika Kusini ikiranda kwenye anga la eneo la Marikana ambapo ilifanya kazi ya ziada kuwasambaratisha wachimba migodi wanaoandamana ambapo jana eneo hilo lilikumbwa na rasharasha za mabomu ya machozi na risasi za moto.Magari ya vikosi vya polisi ambayo yalisheheni askari wakutosha kudhibiti waandamanaji kwenye eneo la Marikana.
Waandamanaji wakichoma moto ikiwa ni harakati za kuweka vizuizi ili magari ya polisi yasifike kwenye ngome yao.
Miongoni mwa waanndamanaji walikuwemo kinamama ambao wengi wao ni wake wa wafanyakazi kwenye migodi hiyo.
POLISI
wametumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wafanyakazi wa
mgodi huo ambao wamekuwa wakiandamana magharibi mwa mji mkuu wa Pretoria.
Polisi hao walivamia makazi ya wafanyakazi hao mapema
asubuhi siku ya Jumamosi wakikamata silaha mbalimbali zikiwemo mapanga na
mikuki. Serikali ya Afrika Kusini imeapa kukomesha migomo katika machimbo ya
migodi nchini humo.
Migomo hiyo imekuwa ikisambaa na kuendelea tangu polisi
walipowaua wachimba migodi 34 katika mgodi wa Marikana hapo Agosti 16 mwaka
huu. Siku ya Ijumaa baraza la mawaziri lilitangaza kuwa halitavumilia kile
walichokiita mikutano isiyo halali na kutishia kuwanyanganya silaha waandamanaji
hao.
Wanaume kwa wanawake na watoto walitawanyika baada ya polisi
waliokuwa wakisaidiwa na helikopta za jeshi zilizokuwa angani zikirusha risasi
za mpira na gesi za kutoa machozi kwa waandamanaji. Maombolezo wakati wa mazishi
ya wachimba madini waliouawa . Picha za televisheni zilionyesha watu waliokua
na majeraha yaliyochuruzika damu.
"Gari la polisi lilitupita, tulikuwa ni kundi la
wanawake na watu wengine walikimbia. Nilisimama pale nikiangalia na walinipiga
risasi mguuni," Melita Ramasedi aliliambia shirika la habari la Sapa. Wakati
polisi wakiwasili katika eneo hilo waandamanaji walitumia matairi yaliyowashwa
moto kuzuia polisi hao kuingia katika eneo hilo, ripoti zinasema.
Mapema polisi 500 walifanya uvamizi wa makazi ya wafanyakazi
hao mapema asubuhi wakikamata silaha mabalimbali, msemaji wa polisi Thulani
Ngubane amesema. Ameliambia shirika la habari la AFP kuwa polisi waliwakamata
watu 12 ingawaje watano kati yao ni kwa makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya
na sio silaha.
"Popote tutakapoana tabia kama hii ya vurugu na watu
wakijichukulia sheria mikononi kwa kufanya maandamano yasiyo halali, hakika
tutachukua hatua," alisema. "Polisi hawatasita kuchukua hatua.
Tutachukua hatua kama ambavyo tumekwisha anza na tutaendelea kufanya
hivyo."
Maandamano hayo yameshuhudia mamia ya wafanyakazi wakiwa na
fimbo na mapanga wakipita kutoka mgodi mmoja hadi mwingine eneo la Marikana na
maeneo mengine na kutishia yeyote atakayerejea kazini.
Malipo yakataliwa
Wafanyakazi hao wamekuwa wakidai nyongeza ya mishahara
kufikia randi 12,500 kwa mwezi (sawa na pauni 930 au dola za kimarekani 1,500)
kutoka kiwango cha sasa cha kati ya randi 4,000 hadi 5,000.
Mapambano kati ya polisi na waandamanaji hivi Karibuni Mapambano
kati ya polisi na waandamanaji Siku ya Ijumaa wafanyakazi hao walikataa ahadi
ya nyongeza ndogo ya mishahara, ya randi 1,000 kwa mwezi, iliyotolewa na
mwajiri wao kampuni ya Lonmin,wakisema kuwa ni sawa na kuwatukana. Tokea vifo
vya mwezi Agosti katika mgodi wa Marikana, migomo imekuwa ikisambaa katika
maeneo mengine ya migodi nchini Afrika Kusini.
Waziri wa fedha Pravin Gordhan ameonya kuwa migomo hiyo
inaweza kuathiri ukuaji uchumi, ajira na imani ya wawekezaji katika nchi hiyo
yenye uchumi mkubwa barani Afrika. Baadhi ya vyama vya wafanyakazi vimetishia
kuitisha mgomo mkubwa.
No comments:
Post a Comment