Ni kiwanja namba 130/1Kawe beach Dar es Salaam. Waandishi watishiwa mtutu wa bunduki
Kiwanja chenye mgogoro ambacho kinaendelea na ujenzi kwenye eneo karibu kabisa na njiapanda ya Kawe na Mbezi beach. Pichani ni mama Beatrix Mugishagwe anaedaikuwa ni mmiliki halali wa kiwanja hicho ambacho anashangaa kukuta mtu akiwa anajenga hku akiwa ameweka ulinzi mkali. Mwandishi wa blog hii alifanikiwa kupata picha chache kwenye eneo hilo baada ya walinzi hao kuchomoa mitutu ya bunduki na kuanza kuwafukuza waandishi hao, walikuwa wakifuatilia sakata hilo.WAKATI huohuo Beatrix ameripotkituo cha polisi kawe na kupewa RB namba KW/RB/87832012 pamoja na kuandika barua manispaa ya kinondoni kuripoti taarifa za uvamizi wa kiwanja hicho. Juhudi za kumpata mtu anaedaiwa kupoka eneo hilo zinaendelea baada ya kushindwa kupata nambayake ya simu.
Barua iliyowasilishwa manispaa ya Kinondoni na mlalamikaji ambapo manispaa hiyo ilimtaka mlalamikiwa kusimamisha ujenzi lakini aliitii amri hiyo kwa sikumoja tu ya Ijumaa yani jana lakini leo anaendelea na ujenzi kama kawaida.

No comments:
Post a Comment