Baadhi yao waliziba midomo kuashiria kuwa maandamano hayo ni yakimyakimya lakini pia wakimaanisha kitendo cha kuwaua waandishi ni kuwaziba midomo wasiseme.
Mabango yenye ujumbe wa aina mbalimbali yalibebwa na waandamanaji hao.
Hapa igizo la Mauaji ya Mwangosi likiendelea.
Igizo likiendelea pembeni picha ya daudi mwangosi.
Ujumbe wa kupinga mauaji hayo ukibebwa na waandishi hao.
Maandamano hayo yakiwasili eneo la viwanja vya Jangwani.
Ujumbe mahususi wa Chanel ten ni huu hapa kwenye bango.
Wapiga picha wakifokass tukio zima.
Hapa wa Mambo ya ndani Emanuel Nchimbi
Hapa wakimuondosha ili awaache wazungumze yao, akawapa mikono ya kwaheri huku akiondoka.
Kabla hajafika popote kundi la waandishi walewale waliomkataa wakamfuata na hapa wanamuhoji!!! Dah hii ni kali kweli tena yamwaka. aku!! mimi simo nilisogea kutimiza wajubu huu wakukufikishia wewe usie kuwepo ujue yaliyojiri, ukiniuliza alichoongea sijui maana nami sikutaka kusikiliza kwakua alishafukuzwa.
Fusi la mchanga lilikua ndio jukwaa la kupazia sauti, ambapo mkutano huo uliendelea bila vipaza sautu hadi dakika 20 kabla kumalizika mkutano likaingia gari la vipaza sauti vya kukwaruza, haikuwa komedi lakini ndio hali halisi!!, kujipanga muhimu!
Wanachuo wa DSJ yaani Dar es Salaam School Of Journalism nao waliunga mkono maandamano hayo na kuja na mabango yao.
Majembe haya ni zao la DSJ sasa yanakamua vilivyo jijini Dar Salaam, ni Photojournalist wote walivyokutana kwenye maandamano hayo baada yakupotezana kwa siku kadhaa kutokana na mgawanyo wa kazi na maisha.
Wana DSJ wakiwakwenye picha ya pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali.

No comments:
Post a Comment