Rais wa Mauritania, Mohamed Ould
Abdel Aziz pichani, anapelekwa Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa
alipopigwa risasi.
Kabla ya kuondoka kuelekea Paris,
Rais Abdel Aziz alisema kwenye hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni kutoka
hospitali, kwamba ameshafanyiwa upasuaji ambao ulifanikiwa.
Wakuu walisema rais alijeruhiwa
wakati wanajeshi wa serikali waliokuwa kwenye doria, walipofyatulia risasi
msafara wa rais. Inaarifiwa kuwa maafisa wawili wa
jeshi wamekamatwa.
Jenerali Abdel Aziz, ambaye
anaonekana na mataifa ya magharibi kuwa anasimama dhidi ya wapiganaji wa
Kiislamu katika eneo hilo, alichaguliwa mwaka wa 2009, mwaka mmoja baada ya
kupindua serikali.
No comments:
Post a Comment