HUGO SHAVE ASHINDA TENA URAIS. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, October 8, 2012

HUGO SHAVE ASHINDA TENA URAIS.

Rais wa Venezuela Hugo Shavez akishangilia mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Mfuasi wa Hugo Shavez akuwa amevalia picha ya Rais huyo Mshoshalist.
Rais Hugo Chavez ameshinda tena uchaguzi mkuu na hivyo kupata nafasi ya kuiongoza Venezuela kwa miaka mingine sita ijayo, huku viongozi wengine wa eneo hilo wakiusifu ushindi wake na mpinzani wake akikiri kushindwa.
"Idumu Venezuela. Adumu mwasisi Bolivar. Yadumu Mapinduzi ya Bolivar!" Rais Chavez alijitokeza kwenye roshani kuwasilimia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika nje ya kasri ya rais mjini Caracas kushangiria ushindi wa asilimia 54 wa kiongozi huyo mwenye siasa kali za mrengo wa shoto.
Dalili kwamba Chavez angelishinda tena uchaguzi huu zilikuwa zimeanza mapema hata kabla ya Tume ya Uchaguzi kutangaza rasmi matokeo. Wafuasi wake tayari walikuwa wamejazana mitaani, wakishangiria kwa kurusha fashifashi na kupiga mayowe ya "Idumu Venezuela. Adumu Chavez!"
Hata hivyo, wagombea wote wawili walikuwa wameshaonesha kukubaliana na matokeo ya uchaguzi huo vyovyote yatakavyokuwa. Rais Chavez aliwataka wafuasi wake kutulia na kukubali matokeo yoyote yatakayotangazwa.
Capriles akiri kushindwa

Aliyekuwa mgombea wa upinzani, Henrique Capriles. Aliyekuwa mgombea wa upinzani, Henrique Capriles.
Naye Henrique Capriles, aliyeendesha kampeni zilizotoa upinzani mkali wa Chavez, amekiri kushindwa na kumpongeza Rais Chavez.
"Anayejua kushinda anaweza pia kushindwa. Mimi ni mwanademokrasia. Nautambua uamuzi wa umma. Nauheshimu uamuzi huo. Na nampongeza rais wa Jamhuri!" Amesema Capriles.
Katika hotuba yake kwa umma mara tu baada ya kuthibitishwa ushindi, Rais Chavez ameahidi kufanya kazi na upinzani huku akitoa wito wa kuwapo umoja wa kitaifa katika nchi hiyo iliyogawika.
Chavez amesema licha ya kuwa ushindi wake ni wa wazi na kamili, bado anahitaji kumshirikisha "kila mtu kwenye uongozi wakiwemo wapinzani."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here