LEO NI SIKU YA AFYA YA MACHO DUNIANI, WADAU WAADHIMISHA JIJINI DAR ES SALAAM. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, October 11, 2012

LEO NI SIKU YA AFYA YA MACHO DUNIANI, WADAU WAADHIMISHA JIJINI DAR ES SALAAM.

Meneja wa Ushirikiano wa Benki ya Standar Chartered Beda Biswalo, akiwaelekeza wafanyakazi wa benki hiyo njia watakazopita kuandamana kwaajili ya maadhimisho ya siku ya afya ya macho duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo takwimu za tatizo la ubovu wa macho zilitolewa ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Afya bora ya macho na maendeleo ya Taifa sambamba na kauli mbiu hii, ujumbe mahsusi kwa wadau wa Afya ni: Amua kuwekeza sasa katika huduma za macho uepushe gharama za ulemavu wa kuona”.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik, akikata Utepe kuzindua maandamano ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered kwaajili ya maadhimisho ya Siku ya macho duniani yaliofanyoka leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa taasisi ya Brien Holden Vision Istitute wakishirikiana na Standard Chartered kuandamana kutoka Posta  hadi kwenye viwanja vya Biafra kwaajili ya maadhimisho ya siku ya macho ambayo hufanyika kila Alhamisi ya mwanzo ya mwezi wa 10.
Daktari wa Macho akimfanyia uchunguzi mgojwa wa macho Upendo Kisese huku Mkuu wa Mkoa akishuhudia kwenye viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya siku ya macho duniani.
Msimamizi wa Kitengo Cha macho Manispaa ya Ilala Ramadhani Msuya, akimpima mgonjwa wa macho  Ustadh Abuu Yusuph wakati wa Maadhimishohayo ambapo huduma hizo zinatolewa bure kwa siku nzima.

TAKWIMU:
KULINGANA na takwimu za Shirika la Afya Duniani, inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni arobaini na tano (45,000,000) hawaoni na watu milioni mia mbili sitini na tisa (269,000,000) wana uoni hafifu duniani kote. Asilimia 4 ya wakazi wa dunia hii wana uoni hafifu/upofu. Asilimia 90 ya watu wenye upofu ni wakazi wa nchi zinazoendelea.

Jambo la kutia moyo ni kwamba wataalam wamethibitisha ya kwamba asilimia 80 ya matatizo hayo yanayosababisha kutokuona yanazuilika au kutibika.

Hapa kwetu Tanzania inakadiriwa kuwa ni zaidi ya watu 400,000 ambao ni sawa na asilimia 1 ya wakazi wa nchi nzima. Asilimia 3 ya watanzania (takribani watu zaidi ya milioni 1.2) wana uoni hafifu na kila mwaka watanzania zaidi ya 70,000 wanakuwa vipofu kutokana na sababu mbalimbali.


Upofu huu husababishwa kwa kiwango kikubwa na magonjwa au hali zifuatazo:-

1). Cataract (mtoto wa jicho) 50%
2). Ukungu wa kioo cha jicho (cornea) 20% - ambao
     husababishwa na trachoma au upungufu wa Vitamin A
3). Glaucoma (presha ya macho) 10%
4. Matatizo mengine - 20%. (Kisukari, magonjwa ya Retina
    refractive errors na low vision).

Hali ya huduma za macho Mkoa wa Dar es Salaam:

Historia fupi ya huduma za macho katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Huduma ya macho ilianzishwa mwaka1970 - Hospitali ya Muhimbili. Mwaka1978 ilianzishwa kwenye Zahanati ya Mnazi mmoja. Baada ya hapo huduma zilianza kutolewa Manispaa ya Temeke na Kinondoni mwaka 1990, hatimaye mwaka 1994 zilianzishwa CCBRT.

Mkoa wa DSM una vituo vya huduma ya macho vya serikali 9, binafsi 6, na vituo vingine vya kutoa huduma ya miwani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here