Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa Mahakamani Kisutu.
![]() |
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Sheikh Ponda Issa Ponda (katikati)akiwa kwenye Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo alisomewa mashtaka mbalimbali akiwa na wenzake 59, hata hivyo amenyimwa dhamana na kurudishwa rumande.
|
Na Happy Katabazy
HATIMAYE Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu(T), Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake 49jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam chini ya ulinzi mkali wa wanausalama kwa kosa la uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Shilingi milioni 59.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilishwa mahakamani hapo hati ya kuzuia Ponda asipewe dhamana chini ya kifungu cha 84(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambapo kifungi hicho kinampa mamlaka DPP kufunga dhamana kwa mshtakiwa anayekabiliwa na makosa yanayodhaminika na mahakama inakuwa imefungwa mikono hivyo mahakama inakuwa haina mamlaka ya kuipinga hati hiyo ya DPP hadi pale siku DPP atakapojisikia kuiondoa mahakamani hati hiyo.
Hakimu Stewarty Sanga ameamuru washitakiwa wote waende gerezani hadi Novemba mosi mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya kutajwa.Ulinzi ila kesi ilimalizika salama.
No comments:
Post a Comment