Shirilisho la Ngumi la Kimataifa
(IBF) limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika,
Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, Mtanzania Francis Cheka.
Katika
barua yake aliyomtumia Francis Cheka ya tarehe 28/12/2012 Mwenyekiti wa kamati
ya Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alisema "Tunachukua
fursa hii kukutakia maisha na mafanikio mazuri kama bingwa wa IBF na kumhimiza
kuishi kama bingwa". Cheka atatakiwa kutetea taji lake
katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi wa 6 mwakani dhidi ya mpinzani
ambaye ana rekodi ya mapambano yasiyopungua 15 na mengi awe ameyashinda hususan
mapambano mawili ya mwisho.
Aidha
IBF inampongeza bondia Chiotcha Chimwemwe kutoka Malawi kwa ushupavu wake na
ushindani mzuri katika pambano hilo lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid katika jiji la Arusha tarehe 26 Desemba, 2012.
Imetolewa
na:
Onesmo A.M. Ngowi
Rais
IBF/USBA
Afrka, Ghuba ya Uajemi an Mashariki ya Kati
No comments:
Post a Comment