Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Agness Hokororo akiwasalimia baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa macho. |
Katika kusherehekea sikukuu ya Xmass na mwaka mpya zaidi ya watu 2600 wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wamepatiwa huduma ya tiba ya macho huku 90 kati ya hao wakifanikiwa kupata operesheni na kuweza kuona baada ya kutoona kwa zaidi ya miaka 10.
Wakiwa na furaha na kustaajabu baadhi ya wagonjwa hao akiwemo bi Somoe Omary mkazi wa Kinyope wilayani Lindi aliekuwa haoni tokea mwaka 2002 jana ilikuwa ni siku ya ajabu kwake baada ya kupata msaada wa Tiba ya macho inayotolewa wilayani humo na Taasisi ya kiislamu ya (Bilal Muslim Mission)Tawi la Tanzania Kwa ufadhili wa Mbunge wa Jimbo hilo Kassim Majaliwa
Wakiongea na mtandao huu,Bi Somoe Omary pamoja Bi Hadija Bakari Mkazi wa Mandarawe wilayani humo walitoa shukrani zao kwa kupata tiba na kuweza kuona baada ya kutoona kwa miaka kadhaa
Aidha walimshukuru Mbunge wao wa Jimbo la Ruangwa kwa jitihada zake za kusaidia jamii ikiwemo la kuwaleta wataalamu hao na kuwezesha wao kuweza kuona baada ya macho yao kupoteza Nuru ya kuona kwa miaka mingi na sasa kurudi katika hali ya kawaida.
‘Kwa kweli mimi sina la kusema hakika nina wajukuu zangu watano wamezaliwa nikiwa sioni ila niliwazoea kwa sauti zao lakini leo nashukuru nimewaona na hata kanga zangu ninazovaa nimeziona hata
rangi zake hakika huyu Majaliwa naomba ajaliwe kama jina lake lilivyo Mungu amsaidie’Alisikika Bi Somoe Omary Katika zoezi hilo jumla ya wagonjwa 90 ambao walikuwa hawaoni kabisa wameweza kupata tiba ya macho kwa kufanyiwa Upasuaji na sasa wanaona kama awali
Akitoa taarifa katika mkutano wa Uzinduzi wa huduma hizo uliofanyika jana wilayani,Mratibu wa Taasisi hiyo kitengo cha Macho,Bw Ain Sharrif alieleza kuwa Kufuatia maombi ya Mbunge wa Jimbo hilo ambae pia ni
Naibu wa Waziri wa Tamisemi,Kasim Majaliwa,Taasisi yake ikiongozwa na Rais wake Bw Anver Merali Alibhai,Taasisi hiyo tayari imeshatoa tiba ya Macho kwa zaidi ya watu laki mbili Nchini huku wilaya hiyo
wakifanikiwa kuwezesha wananchi wawili kuweza kuona baada ya kutoona kwa zaidi ya miaka 10
Wilaya ya Ruangwa toka ianzishwe miaka 18 iliyopita ni mara ya kwanza kwa wananchi wake kupata huduma hiyo ya bure baada ya wilaya hiyo kukabiliwa na tatizo la wananchi wake walio wengi kukabiliwa na
matatizo ya Macho na wengine wakipata upofu Taasisi hiyo imeanza kazi hiyo tarehe 22 mwezi huu na itamaliza utoaji wa Huduma hiyo tarehe 27 kurejea Dar es sallam
No comments:
Post a Comment