Habari iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa kundi kubwa la
wananchi wenye hasira kaliWilayani Rufiji leo wamevamia kituo
cha Polisi Kibiti Wilayani humo na kuanzisha vurugu kubwa kufuatia raia mmoja mkazi wa kijiji hicho kudaiwa kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa
ni kutokana na kipigo cha Polisi. Chanzo chetu cha Habari kutoka Kibiti kinatupasha kuwa, kijana huyo aliyefariki kutokana na kipigo hicho afahamikae kwa jina la Hamis Mpondi ambaye mauti
yamemfika wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini
Dar es Salaam na taarifa hiyo ilipowafikia wananchi hao ndipo
wakachukua uamuzi wa kwenda kituoni hapo na kuanzisha vurugu hizo. Habari zaidi zinaeleza kuwa, hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari
Polisi hao zilizopo jirani kabisa na kituo hicho, licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika. Aidha wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini,
Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali
wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti. Inaelezwa kuwa hali imezidi kuwa tete katika eneo hilo huku Polisi wa Kibiti wakiendelea
na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu ya machozi
hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu. tutaendelea
kupeana taarifa zaidi kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
|
No comments:
Post a Comment