HAMAD RASHID ABEBA MZIGO WA HIJABU JITEGEMEE! - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, January 19, 2013

HAMAD RASHID ABEBA MZIGO WA HIJABU JITEGEMEE!

Mbunge wa Wawi kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Hamadi Rashid Mohamed, akizungumza na wahitimu wa kidato cha sita wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari Jitegemee (JIMSA) ya jijini Dar es Salaam jana wakati wa mahafali yao ya 9 tangu kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ambapo jumla ya wanafunzi 42 wamehitimu masomo yao wakiwa wanaume 26 na wanawake 16, kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Bakwata Taifa Rajab Alqushairiyyu na katibu Omary Msinzia. Hamad Rashi aliwaahidi wanafunzi hao kufikisha kwa Waziri wa Mambo ya ndani suala lao la madai ya kuzuiwa kuvaa hijabu kwa wanafunzi wakike kwenye shule hiyo huku shule zingine za Jeshi ikiwemo Makongo na Airwing wakiruhusiwa.

Baadhi ya wahitimu wakike wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
Mmoja wa wahitimu hao akipokea cheti kutoka kwa Mbunge wa Wawi Hamadi Rashid Mohamed ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.
Mbunge wa jimbo la Wawi Pemba Hamadi Rashid Mohamed (aliyemshika mtoto) na baadhi ya maustadh wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wakiislamu mara baada ya mahafali yao.
Hapa akiwa na wahitimu wakiume.
Wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambayo ilijikita zaidi kwenye kuwasihi wajifunze kuishi vizuri na jamii nyingine ambazo wako tofauti na imani yao kwakutumia kauli nzuri.
Kwaumakini wanafunzi hao wakimsikiliza Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed wakati akiwahutubia kwenye mahafali yao.                                                                                                                                       
Changamoto zinazowakabili zilizoelezwa kwenye risala ya wanafunzi hao
Kutoruhusiwa kuvaa hijabu ingawa shule zingine za Jeshi hilo kama Makongo na Airwing wanaruhusiwa kuvaa lakini Jitegemee imekuwa vigumu kuruhusu pamoja na aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi na Usalama Abdurahmani Shimbo kwenye mahafali kama hayo alitoa agizo kuwa wanafunzi wakiislamu waruhusiwe kuvaa hijabu lakini agizo hilo halijatekelezwa. Changamoto nyingine ni ukoseph wa mwalimu rasmi kwa somo la Islamic Knowledge

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here