AKITOA maoni yake mbele ya tume hiyo jana,
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Mstaafu Damian
Lubuva alisema kwamba muundo wa Muungano unapaswa kuangaliwa upya
kikatiba, ili kuondoa malalamiko yaliyopo kwa muda mrefu. Alisema
suala la dola kwa nchi zilizoungana yaani Tanganyika na Zanzibar
linapaswa kutambuliwa ili kila nchi iwe na mamlaka yake kamili.
“Kwa hali ilivyo sasa dola haiko Tanganyika wala
Zanzibar, bali iko kwa Tanzania yote. Jambo hili linaleta manung’uniko
mengi kwani Zanzibar kama ilivyo kwa Bara inahitaji kuwa na dola kamili.
Napendekeza mfumo wa Muungano ufuate matakwa ya
wananchi kutoka kila upande, pia Katiba iainishe mambo ya Muungano ili
kuondoa malalamiko kutoka kila upande,” alisema Jaji Lubuva. Pia
alisema Bunge linapaswa kuendelea na wajibu wake wa kutunga sheria na
kuisimamia Serikali na siyo kufanya kazi za wizara.
Alisema kwa hali ilivyo sasa, Kamati za Bunge
zimekuwa zikitoa maagizo na uamuzi kwa mambo mbalimbali kitu alichosema
kuwa siyo sawa kwani hayo ni majukumu ya Serikali.
Jaji Lubuva alisema kitendo hicho kinaweza
kudhoofisha utendaji wa Serikali, pia hakizingatii mgawanyo wa madaraka
kwa mihimili ya dola. |
No comments:
Post a Comment