 |
Jeshi
la Polisi linaonekana kufanya kazi zaidi kwa mazoea kuliko kuzingatia mafunzo
wanayopewa, pichani ni askari polisi aliyejeruhiwa na wenzake baada ya kupigwa
marungu kwa kutomjua kama nayeye ni askari hadi alipopiga kelele ‘mtaniua mimi
mwenzenu’ ndipo wakamuachia.
Kilichofuata baada ya askari huyo kuachiliwa na
wenzake alimalizia hasira zake zote kwa wanafunzi hao kwa kutembeza kipigo
(mkong’oto) mkali kwa wanafunzi Chuo Cha IFM waliojaribu kutaka kulazimisha
jeshi la polisi kufanya mkutano mbele ya kituo cha Polisi Kigamboni badala ya
kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava Kigamboni bila kujali kuwa wanafunzi
hao walikuwa wakikabiliana na moshi nzito wa mabomu ya machozi lakini pia
walisha kuwa chini ya ulinzi mkali na hakukuwa na sababu yeyote ya kuwapiga
hivyo.
Mbali na askari huyo kulikuwepo na askari wengine wawili akiwemo mmoja wakike naopia waliambulia kipigo hiko. Fuatilia picha za Askari huyo na
matukio aliyofanya .
|
 |
Picha hii inakuonesha kwa karibu namna rungu lilivyompasua Askari huyu, hapa utapata picha kama huyu askari aliyepigwa kidogo tu baadaye akaachiwa ameumia hivi je wale waliopata mkong'oto wapo kwenye hali gani. |
 |
Hapa anazuia damu sehemu aliyopigwa isindelee kuvuja kwa kutumia kitambaa. |
 |
Baada ya kupata nafuu anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi huyo. |
 |
Hakuishia hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na kumpa kipigovile alivyojiskia ili amalizie hasira zake. |
 |
Kumbuka kipigo hicho kinafanyika mbele ya kituo cha polisi huku kukiwa na ulinzi mkali umeimarishwa. |
 |
Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka! |
BAADA
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda
wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao
hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa,
waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka
mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi
wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa
maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo
ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa
na kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa
na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya
utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova
aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya
tarehe 30 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment