MAAFA YA UBUNGO LEO ASUBUHI, Yasababisha hasara ya mamilioni ya shilingi. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, January 21, 2013

MAAFA YA UBUNGO LEO ASUBUHI, Yasababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.


Ukuta wa eneo la ndani ya kituo cha mabasi Ubungo ukiwa umeangukia bajaji tatu na magari zaidi ya 20  ambavyo vyoote vilipaki kwenye eneo linalotumika na watu wanaosindikiza nduguzao, taarifa zinaeleza kuwepo kwa majeruhi  kadhaa ambao wamekimbizwa Hospitali. Imeelezwa Chanzo cha ajali hiyo ni mkandarasi anaeendelea na kazi ya ubomoaji wa baadhi ya maeneo kwenye kituo hicho.

Pichani juu ni baadhi ya magari mbalimbali yalioyoathiriwa vibaya kufuatia kungukiwa na ukuta.
Picha hii inaonesha eneo hilo kwa upanawake lilivyo athirika na tukio hilo nanamna magari na bajaji zilivyo athirika
Baadhi ya wananchi wakishuhudia mabaki ya kuta hizo zilizo haribu magari.
Kutokana na ajali hii kuna baadhio ya watu wamejeruhiwa na kukimbizwa Hospitali.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Afande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi.

Baadhi ya Maofisa kutoka Jeshi la Polisi wakiangalia baadhi ya magari yaliyoathiriwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta mapema leo asubuhi kwenye eneo la kupaki magari,ndani ya kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani.Ukuta huo ulikuwa ukibomolewa na Mkandarasi ikiwa ni hatua za awali wa kituo hicho kuvunjwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi. Picha  kwa hisani ya JIACHIE BLOG.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here