![]() |
Picha hii si yatukio halisi la Mtwara na wala haina uhusiano na tukio hilo. |
ASKARI wa kikosi cha kutuliza ghasia wametanda Mtwara na mabomu
yanaendelea kupigwa tangu majira ya saa tano asubuhi. Nyumba kadhaa zimechomwa
moto ikiwemo nyumba ya Waziri wa Tamisemi Hawa Ghasia pamoja na nyumba kadhaa
zikiwemo za viongozi wa CCM.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mtwara
amesema hakuna aliyejeruhiwa lakini taarifa ya Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza
zinasema mwandishi wa habari mmoja wa mjini Mtwara amepigwa jiwe na kupasuka na
kushonwa zaidi ya nyuzi nane kichwani.
Chanzo cha tukio hilo kimeelezwa kuwa ni
tuhuma za ushirikina kwa diwani mmoja ambae nyumbani kwake wameanguka watu
wanaosadikiwa kuwa ni wachawi, kutokana na tukio hilo kuna baadhi ya watu
wakitaka kutekeleza mambo yao ya kishirikina ndipo mkusanyiko huo ulipovamiwa na
polisi.
Tukio hilo la vurugu zimekua
zikiunganishwa na sakata la gesi kutokana na matamko yao ambayo wanasema
hawataki gesi isafirishwe kwenda jijini Dar es Salaam. Mahakama ya Mwanza
iliyopo karibu na Kituo Cha Mabasi nayonayo imechomwa moto na inaendelea kuteketea muda huu.
Barabara za mji wa Mtwara zinawaka moto
kutokana na vijana wengi walioandamana kuchoma moto matairi ya magari hali
iliyosababisha mji mzima kutawaliwa na moshi mzito.
No comments:
Post a Comment