![]() |
Taswira ya stendi kuu Masasi leo. |
Baada ya kufuatilia kwa undani, na kwa
upana kuhusu swala la gesi ambalo linaendelea kuwa ni mgongano au, ni mgogoro
kati ya Serikali na wananchi wa Mkoa wa Mtwara/Lindi kuhusu ujenzi wa bomba la
kusafirisha gesi kwenda kinyerezi Dar- es –Salaam, tumebaini yafuatayo:-
1. Hakuna Sera ya gesi ambayo
husababisha kupatikana Sheria baada ya kupelekwa Bungeni na kuidhinishwa bali
kilichopo ni rasimu ya sera ambayo haina ushirikishwaji wa mawazo ya wananchi
wa Mkoa wa Mtwara na Lindi, ambako vyanzo vya gesi hiyo ipo.
2. Elimu kuhusu gesi na manufaa yake kwa
wananchi haikutolewa ili kujua haki zao kwa madhara yatokanayo na (Uvunaji)
uzalishaji wa gesi hiyo,
na jinsi watakavyonufaika.
Chama cha Mapinduzi katika Ilani yake ya
uchaguzi ya mwaka 2010 inatamka wazi katika Ibara ya 63 kifungu cha H na K juu
ya gesi ya Mnazibay Mtwara na Songo songo Kilwa, Lindi kuhusu umeme wa
(240 MW)
Kinyerezi na (300MW) Umeme wa Mnazi bay Mtwara……
-Vifungu hivi vinafafanua:
• Gesi ya Mnazi bay itakuwa kwa ajili ya
Mitambo ya kuzalisha umeme ambayo itajengwa Mtwara (300MW)
• Mitambo ya kuchakata gesi kujengwa Mtwara
• Ujenzi wa viwanda Mtwara ili malighafi
itokanayo na gesi itumike kutengeneza mbolea, plastic
vikiwemo na viwanda vya
Cementi
2. Gesi ya Songo songo inafafanua wazi
kuwa gesi hiyo itapelekwa Kinyerezi . Dar –es –Salaam kwa madhumuni hayo hayo.
• Kuendeleza viwanda mbali mbali
• Kuzalisha umeme (240 MW)
• Kuchakata gesi kwa kujenga mitambo
Katika ahadi ya Rais wa Jahuri ya
Muungano wa Tanzania alizotoa wakati wa Kampeni za uchaguzi
katika hotuba yake
ya tarehe 29/10/2010 alitamka wazi kuwa Mkoa wa Mtwara uwe tayari kwa maendeleo
makubwa ambayo yanakuja kutokana na gesi iliyogunduliwa katika Mkoa wa Mtwara
huko Mnazi bay
Alimainisha/aliainisha juu ya viwanda
mbalimbali vitakavyojengwa hapa mkoani vya mbolea,cement,
plastic n.k na
kuwataka wananchi wajiandae kupokea maendeleo hayo kwa kujenga nyumba nzuri
zenye sifa kwa ajili ya wageni. Pia wawasomeshe watoto wao ili wawe na elimu ya
juu na kupata ajira
katika Makampuni yanayokuja.
Hata baada ya uchaguzi Rais wetu
alipokuja kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa
kumchagua, alitamka tena
katika hotuba yake akisisitiza ahadi yake ya kujenga viwanda ambavyo
vitaleta
maendeleo kwa Mikoa ya Kusini na kusababisha ajira kwa wana kusini, na kuagiza
kwa Meya
wa Manispaa Mtwara/Mikindani kuwapa maeneo ya kujenga viwanda hivyo,
kwa kile kilichoonekana kukosa maeneo ya ujenzi huo kwa makampuni hayo. Ahadi
hizi alizozitoa kwa wananchi kwa ujumla wao wamezipokea na kuendelea kuzifanyia
kazi.
Chanzo cha Matatizo: Mara baada ya
kuonekana kile walichokitarajia wananchi wa Mkoa wa Mtwara
kwa kutumia gesi ya
Mnazi bay kuleta maendeleo yao kuwa imeamriwa kusafirishwa kwa bomba na
kupelekwa Kinyerezi Dar –Es –Salaam ili kuzalisha umeme na kuchakata gesi na
mitambo hiyo iwe huko.(Mgeuko wa Ilani ya Uchaguzi, na kutozingatia ahadi zake
mwenyewe Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuwa kinyume na kauli za
usemi wake mwenyewe kwa kukitangaza
kituo cha Kinyerezi kuwa ni sehemu ya
mitambo ya gesi ya Mnazi bay-Mtwara na Songosongo-Lindi
na kwamba bomba hilo litachukua
miezi (18) mpaka kukamilika kwake, kwa matamshi haya ndiyo yaliyoleta hasira na
chuki kwa wananchi wa Mtwara/Lindi kwa ujumla.
Hali hii imewafanya wananchi wa Kusini
kutokuwa na Imani na Serikali na viongozi wake wahusika na sakata hili la gesi
kwa semi mbalimbali za viongozi hawa-Mfano.
(1) Kwa hali yoyote gesi lazima itoke
Mtwara (Kwa gharama yoyote ile) kwa kukubali ama kutokubali itakwenda Kinyerezi
kwa bomba
(2) Kuitwa wahaini wananchi wa Mkoa wa
Mtwara kwa kuandamana
(3) Kuitwa wajinga, hawakusoma na kuwa
watu wa vijiweni wasio na elimu ya gesi
(4) Nitafanya lolote hata kama
nitalaumika na Mataifa mengine lakini wapo watakaochekea yatakayotokea na kauli
zinazobadilika kila kunapokucha.
(5) Usemi wa kuigawa nchi vipande
vipande
Viongozi hawa hawajui kuwa chanzo kipo
kwao wenyewe, kwa kutozingatia kuwa wananchi hao ambao hawana elimu kama yao
wanao upeo mkubwa wa kufikiri na kutoa maamuzi kama wanavyotoa wao….
Mfano.
(1) Gesi haitoki Mtwara
(2) Tupo tayari kufa wote kwa ajili ya
gesi
(3) Haiwezekan mitambo ya aina zote
-Kufua umeme
-Kuchakata gesi
-Kunufaisha viwanda vya Dar-es-Salaam
kwa gesi yetu
-Mikataba ya gesi ya Mnazibay kufutwa
ili kuanzisha mikataba iliyo na manufaa kwa Mkoa wa
Mtwara na wananchi wake.
(4) Kwa nini bomba la gesi kujengwa kwa
muda wa miezi 18 na bara bara kwa miaka 51 ya uhuru haimalizwi kujengwa. Je
kwenye gesi kuna nini nyuma yake.?
Hiki ni kiini cha matatizo yote kwa
wananchi wa mkoa wa Mtwara kuandamana na mikutano mbalimbali ya kuhamasisha kutokubali
gesi kuondoka Mtwara
Nukuu za Wananchi wa Mkoa wa
Mtwara/Lindi
1-Kung’olewa kwa Reli
2-Kung’olewa kwa mashine za maji Newala
na kupelekwa Dodoma.
3-Kung’olewa kwa taa za kuongoza ndege
uwanja wa Mtwara na kupelekwa Uwanja wa KIA Moshi
4-Kuondolewa kwa Mtwara Korido
5-Kuwekezwa kwa bandari ya Mtwara kwa
muda usiojulikana inaonyesha jinsi Serikali na viongozi wake wanavyohujumu
Mikoa ya Kusini na wananchi wake kwa ujumla.
-Wananchi wa Mkoa wa Mtwara na Lindi
wamefikia ukomo sasa wa kutengwa kimaendeleo, kimazingira na kutendewa uonevu
wa makusudi na kilio chao cha mwisho ni hiyo gesi ambayo kauli mbiu yao ni GESI
HAITOKI MTWARA KWA BOMBA KWENDA KINYEREZI DAR-ES-SALAAM.
-Wananchi wote wameungana juu ya
kuitetea gesi kutoka Mtwara, badala yake Serikali ifuate mikataba ya kwanza
inayohusu gesi ya Mtwara pamoja na Ilani ya uchaguzi ya CCM ifuatwe na Rais
atekeleze ahadi zote alizotoa hapo kwanza na afute kauli yake ya kupeleka gesi
Kinyerezi, na wala Serikali isitumie nguvu katika swala zima la gesi ya
Mnazibay Mtwara.
TAMKO LA UMOJA WA MAKANISA YA
KIPENTEKOSTE –P.C.T MKOA WA MTWARA
1. P.C.T kwa kuzingatia mwono uliopo wa
hali tete yenye mwelekeo wa kumwagika damu na kuigawa nchi vipande vipande na
kuondokewa amani, yafuatayo yafanyike
• Serikali isitishe mpango wake wa
kuondoa gesi kutoka Mnazi bay Mtwara kwa kuisafirisha kwenda Kinyerezi Dar –es
Salaam kwa bomba.
• Mitambo ya kuchakata gesi ijengwe
Mtwara ili gesi isafirishwe kama mazao ya gesi na mabaki yake kutumiwa katika
viwanda vya mbolea na plastic.
• Mitambo ya kuzalisha umeme ijengwe
Mtwara na kusafirisha umeme na kuunganisha gridi ya Taifa.
• Viwanda vilivyoahidiwa vya
mbolea,plastic,cemet n.k vianze kujengwa sasa na isiwe propaganda tu ya kisiasa
toka kwa viongozi kwa kuondoa dhana iliyotokea huko nyuma ya kuonekana Kusini
ni ukanda wa vita usiendelezwe.
Mfano kule Kilwa Lindi ambako ahadi ya
kujenga kiwanda cha mbolea kwa gesi ya Songo songo mpaka leo hakijajengwa kwa
kuwapatia nafasi ya ajira na kujiajiri kutokana na viwanda hivyo
• Serikali iwe sikivu kwa kilio cha muda
mrefu cha wananchi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi ambako vyanzo vya uchumi wa gesi
vipo kwa kutekeleza madai yao, kwa kuwa hawapingi kupelekwa umeme gridi ya
Taifa na kuuza gesi iliyochakatwa tayari kwa kuliingizia Taifa mapato.
• Serikali ikamilishe sera za gesi na
mafuta na kupatikana sheria ambayo italinda mikataba yote inayofanywa na
serikali juu ya gesi na kulinda wananchi wa eneo husika mikoa ya Mtwara na
Lindi kwa madhara yanayotokana na gesi kwa kuwashirikisha kutoa mawazo yao.
• Mazungumzo yafanyike kati ya Serikali
na wananchi katika kupata ufumbuzi wa swala la gesi kwa njia ya Amani na wala
isitumie nguvu zilizonazo kwani kufanya hivyo ni kuleta maafa yasiyo ya lazima
kwa Taifa.
• -Serikali isisikilize wabunge wadanganyifu
ambao hawana makubaliano na wananchi katika majimbo yao wanayotoka, ambao
huchochea mgogoro huu kwa lengo lao binafsi.
• Viongozi ambao wametoa matusi kwa
wananchi wafute usemi wao kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara ambao wamewaita
wahaini kwa kuwaomba radhi bila masharti yeyote kwani semi hizo huleta chuki,
uhasama, na matengano katika nchi, na kusababisha nchi isitawalike.
• Serikali ya Chama Cha Mapinduzi
itekeleze Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 Ibara 63 Kifungu H na K ambavyo vipo
wazi, hasa kwa kuzingatia kuwa sera zinazotekelezwa sasa na Serikali ni zile
zote zilizoandikwa kwenye Ilani ya uchaguzi.
• Serikali irudishe tumaini kwa wananchi
wa Mikoa ya Kusini na amani inayoonekana kutoweka kwa matamshi yanayoashiria
kumwagika kwa damu bila kujali kuwa nchi ilipatikana bila kuwaga damu.
• Serikali iwatambue wananchi wa Mikoa
ya Kusini kuwa wana haki ya kutimiziwa matakwa yao kama wananchi wa mikoa
mingine kwa kupata maendeleo kutokana na vyanzo vya uchumi vilivyopo katika
maeneo yao.
-Sisi viongozi wa dini tunamwomba Mungu
awape hekima viongozi wetu wa Serikali kwa sababu wamepewa dhamana na Mungu
kuliongoza Taifa.
-Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza,
bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza Methali 11:3
-Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa
kinywa chake, bali wenye haki watapona kwa maarifa. Methali 11:9
Imesainiwa na
BISHOP C. CHILUMBA
MWENYEKITI MKOA
PAMOJA NA:-
PASTOR SELEKWA
KATIBU PCT- MKOA WA MTWARA
Nakala:
• Mwenyekiti PCT Taifa-Dar –es –Salaam
• Maaskofu na Wachungaji wote wa PCT
Mkoa wa Mtwara.
No comments:
Post a Comment