DK.SHEIN ASHIRIKI KWENYE MAULID TUMBATU. - RAHA ZA PWANI
Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 11, 2013

DK.SHEIN ASHIRIKI KWENYE MAULID TUMBATU.

Responsive Ads Here
IMG_9255
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi maalum kutoka kwa mwanafunzi Mohamed Haji Mohamed, iliyotayarishwa na wazee wa Tumbatu Jongowe wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad (SAW), yalipofanyika jana.
IMG_9207
Wanafunzi wa madrasatul Maamur ya Tumbatu Jongowe wakisoma Qaswida wakati wa maulid ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika jana katika zawia ya kijijini hapo.
IMG_9210
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (wa pili kushoto)  akitiliwa marashi wakati wa kumswalia Mtume Muhammad (SAW), yalipofanyika Maulid huko  Tumbatu Jongowe jana, alipohudhuria akiwa mgeni rasmi,pamoja na viongozi na wamini mbali mbali wa Dini ya Kiislamu.
IMG_9182
Baadhi ya Akina Mama wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa nje ya zawia ya kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo.
IMG_9159
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa katika zawia ya  kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad