Alizaliwa 1971, Brooklyn, USA. Alikuwa ni Myahudi na mmoja wa wafuasi wa Satmar (imani fulani ya Kiyahudi). Jina lake la mwanzo ni Joseph Cohen. Ameishi Marekani lakini mwaka 1998 alitembelea Israel. Cohen na familia yake yenye mke (Lona) na watoto wao wane walikwenda kukaa katika makazi ya Ghosh Gatif ndani ya ukanda wa Gaza, lakini baadae wakaenda Netivot, jiji dogo lililopo kusini mwa Israel.
Kukutana kwa Cohen na Waislamu kulianza baada ya safari zake za mara kwa mara katika soko la Yerusalem kwa ajili ya shughuli zake za kazi. Ni hapo ndipo alipoanza kutangamana na baadhi ya Waislamu wanamume na baada ya muda alianza kuisoma Qur’an iliyotafsiriwa kwa Lugha ya kiengereza. Kidogo kidogo akaanza kuwaona wayahudi kama wabaguzi, na akaamua kuwa Muislamu baada ya kuisoma Qur’an. Akiongea na Channel 10 TV, Cohen alisema:
“Siku nilipofungua Qur’an kwa mara ya kwanza sikuweza kuiweka chini,…vile Qur’an inavyowakosoa Wayahudi ni stahiki na sio kwa chuki, kwani Allah alitaka atuonyeshe sisi Wayahudi jinsi ya kujirekebisha na kurejea katika kuabudu Mungu mmoja wa kweli.”
Baada ya mwamko huo mkubwa wa kiroho, Cohen akamwambia mkewe ambaye ni myahudi mkubwa kutoka Marekani kuwa anataka kuwa Muislamu. Nilimwambia, “Sikiliza mke wangu, ujue nakupenda sana na inabidi niwe mkweli na muaminifu kwako…nimeisoma Qur’an na nakubali kila kitu kinachosemwa ndani yake, na kama nikiendelea kusema kuwa dini yangu ni ya Kiyahudi basi ntakuwa nadanganya.” Na kweli alibadilisha dini na kubadilisha jina lake kuwa Yousef mohammed Al-Khattab.
Mkewe ambaye alishtushwa na uamuzi ule alisema, “Wiki mbili baada ya kusilimu kwa Khattab, nikaamua na mie kuisoma Qur’an, na nikaona maswali yangu yote yakipata majibu!” Lona na watoto wao wanne: Rahmaim Shalom (11), Hasiba (9), Ezra (7), na Afoadia (5) wakabadili dini kutoka katika dini ya Kiyahudi kwenda katika Uislamu. Mke alibadili jina na kuitwa Gamar. Watoto wanasoma shule ya Kiislamu na wanazungumza Kiarabu bila tatizo lolote na baba yao yuko katika hatua za juu katika kujifunza Kiarabu. Watoto wao wanasoma Qur’an, kitabu cha sasa cha Waislamu badala ya Taurat, mwenzake Qur’an wakati wa Musa.
![]() |
Jazakh Llah Khaira. |
Khattab alisema pia kuwa kwake Muislamu kulichangiwa na utafiti wake mkubwa alioufanya katika intanet. Alikutana na Muislamu katika mtandao na wakaanza kuchangiana mawazo ili kudadisi na kutafuta dini ya haki. Alikutana pia na wanazuoni wa kiislamu pale Yerusalem ambao walimuelezea vizuri masuala yaliyomsumbua kuhusu Uislamu.
Khattab anasema kwamba yeye ameshika Sunnah (njia) ya Mtume Muhammad na anafata madhehebu ya Ahmed bin Hambal. Sanjari na hilo, amejifunza dini kutoka katika vitabu na Fatawa (sheria za dini) kutoka kwa wanazuoni mashuhuri wa kiislamu kama vile sheikh Abdul-Aziz bin Baaz, Sheikh Nassir Al-Deen Al-Albani, Sheikh Mundhir, na Sheikh Qasim al-Hakee. Alipoulizwa kuhusu kuacha ufuasi wake mkubwa wa Kiyahudi na kuingia katika Uislamu akiishi Gaza akifanya shughuli za Kiislamu, jibu lake lilikuwa, “Niliishi Gosh Gatif kule Gaza, nachukiwa na Israel kwa sasa, kwa sababu ya Uislamu wangu, na sababu ya kuwa Muislamu si jengine bali kuabudu Mungu mmoja wa kweli.” Badala ya kusaidia chama cha kidini na siasa cha Kiyahudi kiitwacho Shas, Khattab sasa anasaidia chama cha Kiislamu kiitwacho Hamas. Hii ni kutokana na ripoti iliyotolewa na Isreal Tv. Anaamini dola ya Kiislamu ije isimamishwe pale katika maeneo ya Izrael na Palestina. Anakataa kuita lile eneo ni la Izrael anaamini na kuliita ni eneo la Palestina.
Xxxxxxx
ukija kuongelea kuhusu Osama bin Laden, Khattab anamuona
Muislamu mwenye juhudi. Haamini kama Osama anahusika na mashambulizi ya
Septemba 11 kule New York. Khattab ni katika wanaoamini kuwa ule ni mpango wa
wenyewe na anashutumu sera za mambo ya nje za Marekani kwa kusingizia ugaidi. Japokuwa
anapingana na maono mengi ya kimagharibi, Khattab katu huwa hatetei ugaidi wa
aina yoyote. “Kubadilika kwake kutoka Myahudi Mmarekani na kuwa Muislamu safi
kunampa dhamana ya kuhubiri mahubiri ya kuwasema wayahudi kuliko wenzake wasio
wayahudi,” Alisema Rabbi Tovia Singer.
Kubadili dini kwa Joseph Cohen, ni kudhihirisha wazi aya ifuatayo ya Qur’an:
“Katika watu waliopewa Kitabu wako wanaomuamini Mwenyezi Mungu na yaliyoteremshwa kwenu na yaliyoteremshwa kwao, kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu. Hawaziuzi Aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo (ya kidunia. Kwa hivyo wamesilimu). Hao wana ujira wao kwa Mola wao. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.” [Q 3:199]
![]() |
Naam! |
No comments:
Post a Comment