Kazi ya kuvunja jengo la ghorofa 16 lililoko kwenye Mtaa wa Indiragandi ambao umefungwa karibu na barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam imeanza jana. Uvunjaji huo unatarajiwa kufanyika kwa muda wa miezi mitatu.
| UBOMOAJI wa jengo la ghorofa 16 lililopo Mitaa wa Indiragandi na Morogoro jijini Dar es Salaam umeanza leo, na kushuhudia mtaa wa Indiraandi ukiwa umefungwa kuzuia magari yasipite. | Akizungumzia ubomoaji huo jana Ofisa habari Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, alisema utekelezaji wa kuvunja ungeanza mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kiutawala moja wapo likiwa kupata mkandarasi. | Hata hivyo tayari mkandarasi wa Kampuni ya Patty Interplan Limited kampuni ya Kizalendo kwa ajili ya utekelezaji wa ubomoaji huo alishapatikana na ameanza kazi rasmi leo. | Watu ambao wapo karibu na jengo hilo tayari wameshahama kwa muda na biashara zote zilizopo katika eneo hilo zimefungwa pamoja na barabara kwa muda ambapo hali halisi kwenye eneo la tukio ilionekana kuwa ya utulivu huku wananchi wakiepuka kupita eneo la karibu na jengo hilo. | Baadhi ya wananchi walioshuhudia ubomoaji huo walikuwa na maoni tofauti, huku wakisemakuna haja ya kufanyika kwa ukaguzi wa majengo yanayojengwa na mengne yaliyojengwa miaka ya hivi karibuni. | “Majengo mengi tumeshuhudia yamejengwa kwa kiwango dhaifu hii ni kutokana na serikali iliyopita kuwa dhaifu na si jengo hili tuu bali yapo mengi”.alisema Ali Pipi. | Kwa upande wake Mrisho Rashidi(34)mkazi wa Kiwalani alisema ubomoaji huo uendelee ili kuepusha athari. | BOMOABOMOA KWENGINEKO. | Bomoa bomoa pia inaendelea katika Manispaa ya Temeke ambapo katika barabara ya Jet Club Rumo nyumba zilizojengwa kwenye ramani ya barabara zimebomolewa. | Katika eneo la Yombo Buza wananchi wameanza kubomoa wenyewe baada ya tangazo lililotolewa kwa wale waliojenga kwenye eneo la barabara.Wananchi hao wengi wao waliojenga mabanda ya duka pembezoni mwa barabara wameanza kubomoa wenyewe kupisha upanuzi wa barabara. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment