Shabiki wa Simba akifungua Shampain na kumwagia mashabiki wa timu hiyo mbele ya Jengo la Klabu hiyo. |
Hivi ndivyo mitaa ya Msimbazi ilivyoamka leo.
Wengine walitoka vyumbani kuangalia mziki wa Simba, wakatoa hi!
Wengine kando ya barabara wakicheza wimbo maarufu wa Young D, Dada Anaolewa.
Hawa nao ni sehemu ya Shamra shamra hizo kila mtaa walipo pita Simba, hapa ni eneo la Faya, mashabiki waliotoka ndani wakiwapa big up simba.
Yani kila Flate wakigombea kuchungulia japo waone 2.
Mashabiki wa Shibam Magomeni 'Shibam' waliandaa mapokezi maalum ya kumuenzi mafisango nao wakawapokea hivi.
Shibam waligusishwa kombe kiduchu iliwalibusu wakaligombea.
Kipenzi cha mashabiki wa Simba Juma Kaseja akiliangalia Kombe nae baada ya kujiunga na msafara huo maeneo ya Usalama Magomeni Mapipa. Juma Kaseja Nyoso na baadhi ya wachezaji wengine walijiunga njiani kutokana na kuwepo kwenye kambi ya timu ya Taifa kujiandaa na michezo ya kimatifa.
'Migomigo tunapitaaa..........mnatuona,' wakiimba mashabiki na wachezaji wa Simba.
Hapa Mashabiki wa Mbagala wanapokea Msafara.
Namna mashabiki wa Simba Mbagala walivyopokea Msafara huo.
Jamani Simbaaaaaaaaaaa
Waooooooooooo Karibuni Mbagalaaaaaaa
Na sisi tumooooooooo!
Baadhi ya Mashabiki wa Simba Mbagala walivyo lipokea kombe hilo na kulinadi.
Wachezaji walitengewa eneo maalum!
Alama hii ya vidole vitano ndiyo iliyoshamiri mitaani kote hadi ndani ya Dar Live, ikimaanisha ushindi wa goli tano walizomfunga Yanga wakati wa mchezo wao wa mwisho wa Ligi.
Burudani kama kawa kila shabiki alijimwaga.
Mashabiki waenzi zileeeee nao walikuja kuwakilisha wenzaoo!
Nani Mshindi?
Waenzi zile waliongezeka.
Walemavu nao wakapewa msaada wakuingia nda kulia ni Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga akisaidia kumbeba mlemavu huyo. |
Raha ya Ushindi nhiii basi tufurahi!
Mwisho:
Na Philemon
Solomon
SOMO la Tehama Katika shule za msingi
limeionekana kuwa ni somo linalopendwa na
wanafunzi wa shule za msingi za serikali lakini wanakuwa hawalifurahii
kutokana kutokuwa na Elimu hiyo kwa vitendo.
Changamoto hiyo inayozikumba karibu
shule zote za
msingi Nchini inajaribu kutatuliwa na Shirika lisilo la kiserikali
lijulikanalo kama
Fahamu Company lenye makao yake jijini Dar
es Salaam
isipokuwa wanakosa ushirikiano kutoka kwa serikali.
Akizungumza na Waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam
Afisa utawala wa Shirika hilo Salmin Kisamo alisema kuwa, wameamua
kufundisha
somo hilo kwa shule zote za msingi ili kuwafungua wigo wa uelewa wa
wanafunzi
katika sayansi ya klutumia Kompyuta.
Kisamo aisema kuwa, katika uchunguzi
mdogo walioufanya
wamegundua kuwa waoto wengi wa shule za msingi hasa za serikali hawana
uelewa
katika somo la Tehama kwani wanakosa walimu wa kuwafundisha pamoja na
vitendea
kazi ikiwemo Kompyuta pamoja na simu.
Alisema, kwa kuanza kufundisha somo
hilo tayari wameanza na shule mbili ambazo ni
Mapinduzi pamoja na Gilman Rutihinda zote za Manispaa ya Kinondoni
jijini Dar
es Salaam.
“Tumeanza na kufundisha shule mbili tu
lakini tunampango wa
kuendeleza mradi huu katika shule zote za msingi Nchini Tanzania hivyo
tunaioma serikali
iingize mkono wake kusudi watoto wetu
waende sambamba na tecknolojia ya kisasa ambayo ni Compyuta”, alisema
Kisamo.
Alienderlea kusema kuwa, kwa sasa
wanawachangisha wazazi wa
watoto wenye mwitikio na mradi huo kiasi cha shilingi 3500 kwa mwezi
ilki
wapate pesa za kuwalipa walimu wanaofundisha somo hilo pamoja na
kurekebishia vifaa
wanavyotumia.
Hata hivyo Kisamo alkiserma kuwa ni
wazazi wacheche tu ndio
wenye mwtikio na wanao lipa fedha hizo kwani sio kila mzazi anauwezo wa
kulipa
fedha hizo.
Kisamo
ameitaka serikali kusaidia kutatua changamoto
waliyonayo ikiwemo uhaba wa Kompyuta ambapo kwa sasa wana kompyuta 36 tu
za
kufundishia wanafunzi zaidi ya 3000 pamoja na fedha za kuweza kuwalipa
walimu
wa kufundisha somo hilo
kwani wazazi hawana uwezo wa kulipa 3500 kwa mwezi.
Nao wanafunzi wanaofundishwa masomo
hayo wameiomba serikali
iwasaidie katika kuongeza vifaa na pia wameonekana kulifurahia somo
hilo.
Mwana funzi aliyejitambulisha kwa jina
moja la Suzan alisema
kuwa anawaomba wazazi wawe na mwamko kwani
nao
eanataka kufanana na wanafunzi wa shule nyingine zisizo za serikali.
MWISHO
No comments:
Post a Comment