AKIONEKANA kama ni mtu mwenye busara mtu mzima kiasi cha miaka 45-50 alimpora mfuko wa pesa muhindi mmoja eneo la Posta jijini Dar es Salaam na kukimbia nazo hali iliyozua mtafaruku na pirika pirika za kumkimbiza.
Mtuhumiwa akipanda gari la polisi. |
Mtuhumiwa akipanda gari la polisi. |
Kijana Mmoja ambae alijitambulisha kwa jina la Castory Dickson alisema pamoja na jamaa huyo kukimbia na mifuko hiyo ya pesa alifanikiwa kumkabidhi mfuko mmoja wa pesa dereva wa daladala ambae hatahivyo inaaminika hawafahamiani kutokana kukifanya kitendo hicho baada ya kuzidiwa na watu.
Panda baba twendeeeee. |
Wakati matukio hayo yote yanatokea hakukua hata na askari walikuwa wakifuatilia hivyo baada ya jamaa hiyo kukimbilia jengo la Hadees watu walimfuata na kumnyang'anya pesa zote alizokuwanazo na kuondoka nazo. Hata hivyo kiasi cha pesa kilicho ibwa bado hakijafahamika hadi sasa.
Raha za Pwani ilishudia jamaa huyo akipandishwa kwenye gari la Poilisi, mara baada ya kwenda kumpekua nakukuta hana pesa hata shilingi badala yake wamemkuta akiwa amechaniwa nguo zake ikiwemo suruali.
WANAOMFAHAMU Baadhi ya watu walioshudia walikua wanadai kumfahamu kijana huyo ambaye walieleza amekuwa akijishughulisha na uuzaji wa vitabu kwa miaka mingi kwenye eneo hilo la Posta na kushangazwa kumuona akikutwa na kadhia hiyo.
Mtuhumiwa akipanda gari la Polisi.
No comments:
Post a Comment