TWIGA STARS WAREJEA NA KAPU LA VISINGIZIO. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, May 28, 2012

TWIGA STARS WAREJEA NA KAPU LA VISINGIZIO.

 Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars akiwasili toka nchini Ethiopia, waliko kwenda kucheza mchezo wa ugenini dhidi ya timu ya nchi hiyo kwenye michuano ya Soka ya Afrika ya wanawake ambapo walifungwa 2-1.


KOCHA Mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa alisema wamepoteza mchezo huo kwa sababu mbalimba moja wapo ikiwa ni hali mbaya ya hewa ambayo iliwafanya wachezaji wake kutojiskia vizuri.


Aidha alieleza sabau zaidi nas kudaikuwa wamefanyiwa hujuma kwa kupuliziwa dawa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hali iliyosababisha kuvikataa vyumba hivyo na kukubaliwa kubadilishia nguo kwenye Korido za uwanja huo.


Hata hivyo pamoja na kuruhusiwa kufanya hivyo lakini muda mfupi tu walipoingia uwanjani kufanya mazoezi walipo rejea walikuta korido yote nayo imepuliziwa dawa hiyo ambayo iliwaondoa nguvu wachezaji.


Taarifa za hujuma hizo zilishuhudiwa na kamisaa wa mchezo na wanataraji kwenye taarifaya kamisaa huyo yatakuwemo malalamiko hayo. Akizungumzia tukio hilo katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kwakua taarifa hiyo itakuwem kwenye ripoti ya kamisaa wao watafanyia kazi na maamuzi yoyote watatoa taarifa ikiwa kuandika malalamiko kwa CAF au kutoandika.
 Wakiwasili
 Tumefungwa lakini mchezo ujao tutajitahidi na tutashinda.
 Wakiwa kwenye basi tayari kuelekea TFF.
  Na hizi nndizo staili za usukaji za wachezaji wetu.

1 comment:

  1. sasa hizo nywele namna hiyo mipira ya kichwa utapigaje?ndio maana tumeshindwa

    ReplyDelete

Post Top Ad

Responsive Ads Here