Msemaji wa Kamati ya Vijana BAKWATA taifa Sheikh Said Mwaipopo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi punde, kulia ni Mhadhiri wa Kiislamu na Mwenyekiti wa taasisi ya Tanzania Talent Islamic Show Ibrahim Bakonzi.
BARAZA la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kupitia msemaji wa kamati ya vijana Taifa Said Mwaipopo imekemea vikali kitendo cha uchomaji moto makanisa Zanzibar na kusema waliofanya vitendo hivyo sio waislamu kwasababu uisilamu hauruhusu kufanywa kwa vitendo hivyo.
Kuhusu kundi la kiislamu la Uamsho linalo dai kuvunjwa kwa muungano Mwaipopo anasema wanayo haki ya kudai kwa sabau hata watanzania bara wapo watu wasioutaka muungano na wanasema uvunjwe lakini madai hayo yanapaswa kufuata taratibu za kisheria. Akinukuu aya za Qurani anasema hata Mtume Mohamad (S A W), aliishi na wasiokuwa waislamu wakiwemo wakristo lakini hata sikumoja akuamrisha kuwachomea nyumba zao za ibada kwahiyo wanaofanya hivyo ni wahuni na Serikali ichukue hatua za kisheria dhidi yao.
Msemaji wa Kamati ya Vijana BAKWATA taifa Sheikh Said Mwaipopo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi punde, kulia ni Mhadhiri wa Kiislamu na Mwenyekiti wa taasisi ya Tanzania Talent Islamic Show Ibrahim Bakonzi.
No comments:
Post a Comment