Aliyewahikuwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mathias Michael Kihaula, pichani juu, leo ameagwa kwa heshima zote hapa jijini Dar es Salaam kwenye ibada iliyofanyika kwenye Kanisa katoliki la Msimbazi Center jijini hapa.
Kihaula mbaye hadi anafariki alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, ameagwa na wananchi mbalimbali kwenye kanisa hilo huku Serikali ikiwakilishwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Wilium Lukuvi Kwaniaba ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Kwa Upande wa Bunge liliwakilishwa na Naibu Spika wa Bunge Mh.Job Ndugai, ambaye alitoa salam za bunge kwa familia.
Kwakuwa marehemu alikuwa Mbunge kwenye jimbo la Ludewa kwa miaka 15 mfululizo na kumwachia kijiti hicho Mbunge wa Sasa Deo Filikunjombe, basi Deo ndiye alikuwa mwenyeji wa shughuli zote za maombolezo kwa kuwa karibu zaidi na ndugu wa familia hiyo pamoja na uratibu wa mambo mbalimbali.
Mwili wa marehemu baada ya kuagwa leo umepelekwa mojakwamoja Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwaajili ya kusafirishwa kesho asubuhi kwa ndege ya Serikali tayari kwaajili ya kwenda Ludewa kwa mazishi hapo kesho kutwa.
Mke wa Marehemu Mathias Kihaule, Bibi Leonia Sijombe (katikati), akiwa ameshika tama wakati ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu mumewake.
Jeneza likiondolewa kanisani tayari kwa safari ya Airport.
Bibi Leonia Sijombo Mke wa Marehemu Mathias Kihale akiuga mwili wa marehemu mumewake.
Mtoto wa Marehemu Mathias Kihaule, Fide Kihaule akitokwa na machozi wakati wa kuaga mwili wa marehemu babayake.
Mama akilia kwa uchungu mbele ya mwili wa marehemu mumewake.
Mh.Lukuvi akiwapa pole familia ya Marehemu Kihaule wakati wa kuaga mwili huo.
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai wakiongozana na Mheshimiwa Lukuvi kuaga mwili wa Kihaule.

No comments:
Post a Comment