CHAMA KIPYA CHA ADC CHA WASILISHA MAOMBI RASMI YA USAJILI WA KUDUMU. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, June 1, 2012

CHAMA KIPYA CHA ADC CHA WASILISHA MAOMBI RASMI YA USAJILI WA KUDUMU.

 Katibu Mkuu wa Chama cha Aliance For Democratic Change (ADC) Kadawi Lucas Limbu, (kulia) akimkabidhi makabrasha ya wadhamini wa chama hicho mwakilishi wa Msajili wa vyama vya siasa nchini Piencia Etanga, ambaye ni Sinior Legal Officer wa tume hiyo, katikati ni Zakia Stephene msaidizi wake.

CHAMA hicho kwa sasa kitakuwa kinasubiri ratiba ya uhakiki wa wanachama hao ambao utafanyika mara tu baada ya kupangiwa ratiba na ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.

Akipokea makabrasha hayo yaliyoandamana na fomu maalum pamoja na barua ya maombi ya usajili wa kudumu, Piencia alisema wamepokea makabrasha yote na wao kama tume watakaa na kuyapitia na baadaye watawapangia tarehe maalum kwaajili ya kufanya uhakiki  wa wadhamini wa wanachama hao.

Awali akikabidhi makabrasha hayo Katibu Mkuu wa chama hicho Kadawi Lucass Limbu, alisema zoezi la kusaka wadhamini hao loiliwachukua kipindi cha miezi miwili lakini wanashukuru kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuvuka lengo.

"Tumefanikiwa sana kwani tumekidhi masharti yote idadi ya wadhamini ilitakiwa angalau mikoa 10 minane bara na miwili visiwani ukiwemo mmoja pemba na mwengine unguja na kila Mkoa usipungue wanachama 200, lakini jambo lakufurahisha tumepata zaidi ya wanachama 16000 kwenye mikoa zaidi ya 16 tuliyopita." alisema kadawi.

"Leo hapa tunawasilisha makabrasha ya mikoa 11, ambapo kati ya mikoa hiyo mitatu ni ya zanzibar na minane ya Tanzania bara ambapo jumla ya wadhamini tuaowasilisha ni zaidi ya elfu tatu ambayo ni ziada ya ile 2000 inayohitajika.

MWISHO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here