Mrembo anaeshikilia taji la Miss Universe Nelly Kamwelu akionyesha uwezowake wa kucheza muziki wa Belly Dance, kwenye harambee aliyoitisha kwa kushirikiana na Mfuko wa Saratani ya Matiti (Breast Cancer Foundation) kwenye harambee iliyofanyika jana usiku.
MREMBO anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2011/2012 Nelly Kamwelu kwa kushirikiana na
Mfuko wa Saratani ya Matiti Tanzania (Breast Cancer Foundation) wamefanikisha ya
harambee ya kuchangia mfuko wa saratani ya matiti iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam
Kwenye mnada huo kulikuwa na mnada wa kito cha Tanzanite ambayo imetolewa maalum na
kampuni ya Richland Resources kwa ajili ya kuchangia mfuko huu, pamoja na picha ya Mrembo wa Miss
Universe Tanzania vilinadiwa na kuuzwa.
Mrembo Nelly Kamwelu toka achukue taji la Miss Universe Tanzania 2011, amekuwa akifanya kazi bega
kwa bega na mfuko wa saratani ya matiti ikiwamo kusaidia kutoa elimu katika shule mbalimbali ili
kupunguza au kutokomeza uwezekano wa kuenea kwa saratani ya matiti. Mfuko huu umepanga
kuendeleza elimu hii kwa shule za mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Iringa, Mtwara na Lindi.
Kwenye hafla hio kulikuwa na maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na wabunifu wa hapahapa
nchini ambao ni Escado Bird, Kemi Kalikawe na Subira Wahure.
Msanii wa Muziki Enika, alitumbuiza na mrembo mwenyewe Nelly Kamwelu alitoa burudani ya kufa mtu na kuwaacha waliohudhuria taabani kwa kucheza burudani ya muziki wa dansi aina ya Belly Dance.
Waliojitokeza kwenye harambee hiyo wakimwangalia Mrembo anaeshikilia taji la Miss Universe Nelly Kamwelu wakati akionyesha uwezowake wa kucheza muziki wa Belly Dance
Watu wajamii na rika mbalimbali walijitokeza.
Afisa Uhusiano ya Jamii na Mazingira wa Tanzanite one Dotto Medad, akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Richland Resource Balozi Ami Mpungwe, Cheti cha Utambuzi wa Mchango wa kampuni hiyo kwenye mapambano dhidi ya saratani ya matiti kilichotolewa na Compass Communications iliyoratibu na kusimamia harambee hiyo.
Mze Sarungi kulia akifuatilia uchangiaji huo.
Nelly akijivunjavunja na miondoko ya Belly Dance.
Wanamitindo nao ilikua sehemu ya burudani.
Wapenzi wa tasnia ya Urembo na mitindo walikuwepo nao kwenye kuchangia.
Msanii Enika akitumbuiza.
Nelly Burudani Zaidi.

No comments:
Post a Comment