Wahanga watahadharishwa.
Wakili wa waathirika hao Dk.Sengondo Nvungi akizungumza na wateja wake kwenye moja ya mikutano yao. |
Na
Mwandishi Wetu
WANANCHI na wahanga wa bomoabomoa kwa wakazi wa nyumba za kota za eneo la
Gerezani, Kariakoo, Dar es Salaam, wametahadharishwa kuacha kuchukua hatua
yoyote kutokana na suala lao kuwa mahakamani.
Wahanga hao wanasubiri kujua kama
watafidiwa kitu chochote kutokana na bomoabomoa iliyowakumba hivi karibuni, na
kupata fidia ya uharibifu na uvunjifu wa haki za wakazi hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Wakili Sengondo Mvungi, anayelisimamia suala hilo, alisema wakazi hao
wanatakiwa kuwa watulivu kwa sasa wakati suala lao likishughulikiwa kisheria,
huku akiwaahidi kulisimamia ipasavyo.
Mvungi, ambaye anatoka katika ofisi
ya mawakili ya South Law Chambers, alisema suala lao litashughulikiwa bila kuwa
na tatizo lolote likisimamiwa na yeye, na kuwasihi wanachi na wakazi wa eneo
hilo kuwa na subira.
Mvungi, alisema taarifa zilizotajwa
na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) kwa wahanga wakapokee
fidia zao linakiuka amri ya Mahakama Kuu, iliyotajwa Juni 28, 2012, na
kuwashauri kutotii agizo hilo. Aidha,
wakili huyo anayewasimamia wananchi wa Gerezani, amewataka kuhudhuria katika
kikao cha pamoja na wakili wao (Mvungi), kitakachofanyika Agosti 11 mwaka huu
(Jumamosi) katika ukumbi watakaoarifiwa na kamati.
Mwisho: