KESI YA MAHALU NA MWENZAKE: - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, August 9, 2012

KESI YA MAHALU NA MWENZAKE:

Hatimaye Mahalu na mwenzake hawana hatia,
Mahalu asema haki imetendeka na ukweli umedhihiri. Furaha na vilio vya furaha vyatawala mahakamani.
Ndugu Jamaa na marafiki wa familia za aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Italy Balozi Costa Mahalu na Mshtakiwa Mwenzake Grace Martine wakiwa na furaha mara baada ya washitakiwa hao kuachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Bi Grace Martine (kushoto) na Balozi Mahalu wakiwa wamezingukwa na waandishi wa habari wakiwa hata kwenye kizmba cha mahakama hawajatoka mara baada ya hukumu hiyo wakitaka kujua namna walivyopokea hukumu hiyo, ambapo Mahalu na Mwenzake wakidaiwa kufanya ufisadi kwenye ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kununua kwa bei iliyochini ya ile iliyopangwa na Serikali.

Mahalu akikumbatiana na mdogowake Miras Rama, mara baada ya hukumu mahakamani hapo.
Punde tu ndugu jamaa na marafiki wakaanza kumtwangia simu na kuwaeleza hivi "ukweli umepatikana na haki imetendeka subiri baadaye tutazungumza 'Ahsante' " alisema mahalu.
Hapa Mahalu (katikati)akizungumza na wakiliwake Mabere Marando (kulia) pamoja na jamaa wengine.
Waandishi nao walikua hawatosheki kila wakati walimtaka aongelee kwa undani namna kesi hiyo ilivyokwenda lakini aliishia kusema "haki imetendeka na nimefurahi kwa hukumu hii".
Pongezi zikaendelea zaidi nje kwenye viwanja vya mahakama hiyo Kisutu jijini Dar es salaam.
Grace Martine akimuangalia kwa furaha wakili wao aliyesimamia kesi hiyo Mabre Marando kulia.

Post Top Ad

Responsive Ads Here