Majambazi Nigeria waua
watu 15 Kanisani.
Majambazi katikati mwa Nigeria
wamewapiga risasi na kuwaua takriban watu kumi na watano katika kanisa moja
wakati ibada ikiendelea.Shambulio hilo limetokea katika kanisailiyo karibu na
mji wa Iokene jimbo la Kogi ambapo majambi walivamia kanisa na kuwafyatulia
risasi waumini.
Baadhi ya watu waliopoteza ndugu zao. |
"nathibitisha watu kumi na
watano wamefariki" alinukuliwa akisema msemaji wa gavana wa jimbo la Kogi
, Jacob Edi.Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo hadi sasa
,lakini kundi la kiislam la Boko Haram limekuwa likilenga makanisa kaskazini
mwa Nigeria na pia maeneo ya kati mwa nchi.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC
nchini humo mashambulizi yalifanyika eneo mbali la kusini mwa Nchi ambako kundi
la Boko Haram halijavami.Kamanda wa jeshi la muungano katika jimbo la Kogi
kanali Gabriel Olorunyomi, alisema kuwa kasisi wa kanisa hilo ni miongoni mwa
watu waliouawa.
Baadhi ya vitu vilivyokamatwa na jeshi la polisi. |
Waumini wengine wengi walijeruhiwa
kwenye shambulizi hilo na kupelekwa katika hospitali mbali mbali kwa mujibu wa
kanali Gabriel Olorunyomi.Maafisa wa utawala wa jimbo hilo, walikuwa wangali
wanawatafuta manusura wengine waliokimbilia usalama wao kwenye msitu uliokuwa
karibu na kanisa hilo.Silaha zilizonaswa na maafisa wa usalama Nigeria
Mwezi Aprili mwaka huu, maafisa wa
ulinzi wa Nigeria walivamia mojawapo ya vituo vilivyoshukiwa kuwa kiwanda cha
kutengeza mabomu mjini Okene na kuwaua takriban watu tisa walioshukiwa kuwa
wafuasi wa kundi la Boko Haram.Mwezi Februari, kundi la Boko Haram lilidai
kushambulia jela moja katika jimbo la Kogi kwa kutumia mabomu na zana nzito za
vita na kisha kuwaachilia huru wafungwa 119.
Hata hivyo mashambulizi mengi
yanayofanywa na kundi la Boko Haram hutokea maeneo yaliyo na waisilamu wengi
kaskazini mwa nchi.Kundi hilo linataka sheria za kiisilamu kutumika katika nchi
hiyo, ambayo watu wengi ni waumini wa kiksristo na ambao wengi wanaishi maeneo
ya Kusini mwa nchi. KWA HISANI YA BBC