Hatimaye ujenzi wa daraja la Kigamboni waanza
rasmi.
Daraja
la Kigamboni likiendelea kujengwa katika bahari ya Hindi eneo la Kurasini
jijini Dar es Salaam. Daraja hilo litakapokamilika litakuwa na njia 6 pamoja na
barabara za juu na kuwa moja ya Daraja kubwa na la kipekee Afrika Mashariki na
Kati.
Waziri
wa Ujenzi Dk John Magufuli (katikati), akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni
akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (mwenye shati jeupe kulia), Mbunge wa
Kigamboni Dk Faustine Ndugulile (wa pili kulia) leo jijini Dar es Salaam.
Daraja la Kigamboni linajengwa na Kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni
214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment