Sababu ni Filamu kumkashifu Mtume Muhammad, Marekani yalaani mauaji hayo.
Balozi
J Christopher Stevens pichani kulia na kushoto ni sehemu ya jengo la ubalozi huo ikiteketea.
Balozi
J Christopher Stevens pichani kulia na kushoto ni sehemu ya jengo la ubalozi likiteketea kwa moto.
BALOZI wa
Marekani nchini Libya ameuawa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa
wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani Mashariki mwa mji wa Benghazi. Balozi
J Christopher Stevens, ni miongoni mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa
kufuatia maandamano kuhusu filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume
Muhammad.
Taarifa zinazohusianaMarekani Idara ya mambo ya ndani
nchini Marekani, imethibitisha tu kifo cha afisaa mmoja wa ubalozi huo ingawa
bado haijataja jina lake. Maandamano ya kupinga filamu hiyo pia yalifanyika
mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa Marekani.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi.
Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo. Serikali ya Libya imetaja shambulio
hilo kama kitendo cha uoga. Ubalozi huo uliteketezwa na watu waliojihami kwa
bunduki kulalamikia filamu moja iliyotengenezewa nchini Marekani ambayo
wanasema inamdhihaki Mtume Mohammed.
Wanamgambo hao wanaoripotiwa kuwa na ufungamano na kundi
la waislamu wenye msimamo mkali walitumia maguruneti ya kurushwa kwa roketi
kuvamia ubalozi huo kabla ya kuiteketeza. Maafisa wa Libya wameiambia BBC
kwamba hali imetulia kwa sasa.
Machafuko hayo ya Libya yalijiri saa kadhaa baada ya
maelfu ya waandamanaji kukusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo
kuelezea hasira zao kuhusu filamu hiyo kumhusu Mtume Mohammed. Kwa wakati mmoja
waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi huo na kuichana bendera ya Marekani
na kurejesha yao.
MWISHO:
No comments:
Post a Comment