Rais mpya anusurika kuuawa kwa bomu.
Rais mpya wa Somalia akihutubia mara baada ya kuchaguliwa hivi karibuni.
RAIS mpya wa
Somalia Hassan Sheikh Mohamud , amenusurika jaribio la kumuua mjini Mogadishu.
Milipuko miwili imetokea nje la lango la makao ya rais
huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati rais huyo alipokuwa anajiandaa kufanya
mkutano na waandishi wa habari.
Taarifa zinasema kuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya Sam
Ongeri pia alikuwa katika hoteli hiyo wakati wa shambulizi. Hata hivyo wawili
hao wamenusurika. Inaarifiwa watu wanne wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment