Malema
awashauri wanajeshi kudai haki zao.
Mwanaharakati Julius Malema akisalimia vikosi vya wanajeshi wa Afrika ya kusini ambao wanakabiliwa na makosa ya kinidhamu.
Mwisho:
Mwanaharakati Julius Malema akisalimia vikosi vya wanajeshi wa Afrika ya kusini ambao wanakabiliwa na makosa ya kinidhamu.
MWANAHARAKATI wa kisiasa nchini Afrika Kusini Julius Malema,
amewashauri wanajeshi wenye manung'uniko kujipanga vyema na kupigania kazi zao.
Malema aliyatoa matamshi hayo kwa wanajeshi wanaokabiliwa na
makosa ya kinidhamu yaliyotokana na maandamano waliyoyafanya mwaka 2009 wakidai
mishahara mizuri na mazingira bora ya kazi.
Kambi za jeshi leo ziliwekwa katika hali ya tahadhari kabla
ya hotuba yake kwa wanajeshi hao, ikiwa ndio mara ya kwanza hatua kama hii
kuchukuliwa tangu kumalizika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Bwana Malema ni mwanasiasa anayeibua mgawanyiko hapa. Hivi
maajuzi alifukuzwa kutoka chama cha ANC na kwa sasa anafanyiwa uchunguzi
kuhusiana na kashfa ya ufisadi.
Lakini hajaondoka ANC kimya kimya. Badala yake ametumia
mauaji ya hivi maajuzi katika mgodi wa Marikana kuanzisha kampeni kali dhidi ya
mabepari nchini Afrika Kusini na kutaka yafanyike mapinduzi ya kiuchumi.
Wengi wanamshutumu kwa kuhusika na ubinafsi mbaya wa
kisiasa, lakini malema anapokea uungwaji mkubwa kutoka kwa jamii za watu
maskini na kimya cha serikali ni ishara tosha kuwa imeshindwa kukabiliana naye.
Manung'uniko ya wanajeshi ni fursa nyingine kwa Malema
kuonyesha ubabe wake na hali ni tete nchini Afrika Kusini.
Hofu iliyopo ni kwamba migomo huenda ikaenea zaidi na kwamba
serikali kwa sasa inazingirwa na migogoro ya ndani huku baadhi ya mirengo serikalini
ikipanga njama ya kumtimua madarakani rais Jacob Zuma.
No comments:
Post a Comment