DARE ES SALAAM KUNAVITUKO!!! - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, September 28, 2012

DARE ES SALAAM KUNAVITUKO!!!

Hawa ni wanafunzi wanaosoma upande wa pili wa jiji la Dar es Salaam almaarufu kwajina la Kigamboni ambao maranyingi hutumia usafiri wa Kivuko hadi kufika huko, lakini iliwavuke wanalazimika kulipa shilingi 50 tu. Lakini miongoni mwao kuna wajanja wanaokwepa kulipa na kupita njia za boda lakini leo hii boda imezibwa na maji hivyo ulihitajika umakini hadi kupenya kwenye uchochoro huo kama wanavyoonekana pichani.

Kama hawaonekani vileee!

Huku kaka zao upande wapili karibu kabisa na soko kuu la samaki la kimataifa Feli wakiwa hawajitambui kwa usingizi majira ya saanane za mchana bila kujali kuwa wamelala kwenye mawe! Hii ndiyo bongo bana hapa mbali na usingizi kuna mengi ya kujifunza moja wapo kua na taifa la watu wanaolala muda wakufanya kazi! lakini lapili ni haja ya kuongeza maeneo ya kupumzika kwani kuna uwezekano waliolala shughuli zao ni za kukesha usiku hivyo hulazimika kulala popotepale.
Baridiiiiiiiiiii wakibarizi upepo mwanana wa bahari.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here