Mmoja wa waandamanaji akipaza sauti leo mjini Benghazi kwenye mkutano uliofanyika baada ya maandamano.
Maelfu ya Walibya wamefanya mhadhara katika mji wa Benghazi,
mashariki mwa Libya, kuunga mkono demokrasi na kuwapinga wapiganaji wa
Kiislamu. Maandamano ya kupinga wapiganaji mjini Benghazi
Waandamanaji waliisihi serikali ya Libya iyapige marufuku
makundi ya wapiganaji ambao wamekataa kukabidhi silaha zao tangu vita dhidi ya
Kanali Gaddafi mwaka jana.
Waandamanaji wanataka serikali izidishe jeshi na polisi, na
walimsifu balozi wa Marekani aliyeuliwa mjini humo juma lilopita. Waliimba
wakati wakiandamana kuelekea medani kuu ya Benghazi.
Muandamanaji mmoja, Faisla al-Naas, alieleza sababu zao:
"Sisi tunaandamana kupinga kundi lenye silaha ambalo
halidhibitiwi na serikali. Wapiganaji hawa wanafaa kujiunga na serikali ili
watu wakae kwa salama. Nchi yetu imekuwa na mtafaruku."
Maandamano mengine ya kuunga mkono wapiganaji yalikuwa
madogo sana.


No comments:
Post a Comment