MKUU WA WILAYA YA KILWA AHAHA KUEPUSHA AIBU YA SENSA. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, September 2, 2012

MKUU WA WILAYA YA KILWA AHAHA KUEPUSHA AIBU YA SENSA.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Pande Wilayani humo juzi alipofika kijijini hapo kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wakihesabiwa kwenye zoezi linaloendelea baada ya wakazi wa kijiji hicho kugoma kuhesabiwa.
 Wakazi wa Kijiji hichowakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Abdallah Ulega.
 Diwani wa kata ya Pande Mikoma Abdallah Oga, akiwakaribisha wananchi kwenye mkutano huo ili waweze kumsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo.
Baadhi ya wazee maarufu kijijini hapo wakifuatilia mkutano huo.


 Said Powa Kilwa.
Baada ya Kaya 256 Wilayani Kilwa Mkoani Lindi  kutia dosari  kwenye mbalimbali zikiwemo za  Tingi,
Kilwa Masoko,  Kivinje na Njinjo wilayani humo kwa kukataa kuhesabiwa  kwa madai ya kutokuwapo kipengele cha dini kwenye dodoso la sense Mkuu wa Wilaya hiyo Abdallah Ulega , anahaha vijijijini kuelimisha wananchi huku kwenye baadhi ya vijiji wanaohamasisha wenzao kupinga sense wakitiwa nguvuni.

Siku moja baada ya kutoa taarifa ya hali ya sense kwenye kikao cha Baraza la Maalum la Madiwani wa

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mkuu huyo alifanya ziara kwenye kijiji cha Pande kuzungumzana wananchi ili wajitokeze kwenye zoezi hilo ambalo likielekea ukingoni kabla ya kuongezwa muda wa siku 7.
Hata hivyo wakazi wakijiji hicho walitoa masikitiko yao kwa mkuu huyo wa wilaya kuwa pamoja na kuwalazimisha kwenda kuhesabiwa lakini wanajisahau mno kwakutokwenda kutoa elimu kwa wananchi jambo ambalo linasababisha sintofahamu kwa wananchi kutokana na kupata taarifa za upande mmoja tu.
Wananchi hao ambao wapo kwenye makao makuu ya tarafa ya Pande pia walihoji kitendo cha kuwanyima haki ya kukutana na tume inayoratibu na kukusanya maoni ya katiba mpya badala yake tume hiyo imepelekwa kwenye kata ambako hakuna uwezekano wa kufika wananchi wengi kutoa maoni yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here