Chief Guest Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel akitoa zawadi kwa Salvina Kibona mshindi wa 4 Miss Eastern zone 2012
Top 3 winners Redds Miss Eastern zone 2012
TOP 5 MISS TALENT
Top 3 winners Redds Miss Eastern zone 2012
TOP 5 MISS TALENT
Mshindi wa tatu wa shindano la
urembo la mkoa wa Pwani Rose
Lucas ameibuka mshindi wa kwanza katika kinyang’anyiro cha kumtafuta
mrembo wa
Kanda ya Mashariki kwa mwaka 2012.
Mrembo
huyo ambaye hakuwa amepewa nafasi yoyote tangu mwanzo
wa ushiriki wake, aliwashangaza mashabiki
na kushangiliwa mara kwa mara alipopanda jukwaani.
Rose Lucas ambaye ni mwanafunzi wa
Chuo Kikuu cha DSM mwaka
wa kwanza anasomea Shahada ya Biashara.
Washiriki wengine walioingia katika tatu 3
bora na ambao pia
wataiwakilisha Kanda hiyo ya Mashariki katika Fainali za Mashindano ya
urembo
ya Redds Miss Tanzania ni, Irene Veda kutoka mkoa wa Lindi na Joyce
Baluhi
kutoka mkoa wa Morogoro.
Maajabu madogo yaliyotokea katika
shindano hilo ni kwamba
washiriki wale wale walioingia hatua ya Tano bora katika shindano dogo
la
vipaji Miss Talent, ndio hao hao walifanikiwa kuingia tena katika hatua
ya Tano
bora ya shindano hilo la kumtafuta mrembo wa Kanda ya Mashariki.
No comments:
Post a Comment