UNAFAHAMU HAPA NI WAPI? Kama hujui usijali lakini lengo langu kubwa kutoa maoni juu ya eneo lililopo jengo hili ili yafanyiwe kazi. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, September 29, 2012

UNAFAHAMU HAPA NI WAPI? Kama hujui usijali lakini lengo langu kubwa kutoa maoni juu ya eneo lililopo jengo hili ili yafanyiwe kazi.

Jengo hili ni jengo la Shule ya Sheria yaani (LAW SCHOOL OF TANZANIA) lipo kwenye viwanja vya posta nyuma ya jengo la Mawasiliano yani TCRA. Eneo hili kwa miaka mingi limekua salama kutokana na kuwekewa uzio wa ukuta mkubwa ilikua ni sahihi kufanya hivyo kutokana na usalama waeneo. Sina hakika kama wameamua wenyewe kuuza au la lakini hoja yangu haipo huko, hoja yangu kama wameamua eneo hili lianze kujengwa basi lingefunguliwa kwa kuondolewa kuta zote na kuweka miundombinu ya kawaida yaani barabara ili watu wanaotoka Sinza kuelekea Chuo Kikuu wasipate usumbufu. Hoja ya pili ni mapori ambayo yamo kwenye eneo hilo yanafuga vibaka na wavuta bangi. Hoja ya tatu kulikua na haja gani yakujenga ukuta ndani ya ukuta?
Eneo lenyewe linavyoonekana kwa picha ya juu ni eneo kubwa ambalo pamoja na umuhimuwake kuwepo lakini kutokana na uzio ulipo linawapa usumbufu mkubwa watu wa Sinza ambao wangependa kwenda Ubungo au Chuo Kikuu kwa miguu. Kwakua eneo hilo limeanza kujengwa basi lingefunguliwa na watu kuanza kupita kama maeneo mengine.
Baadhi ya vichaka ambavyo wavutabangi hujiifadhi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here