ALIYEKOJOLEA QUR-AAN APANDISHWA KIZIMBANI, Waliohisika na vurugu nao 37 wasomewa mashtaka wenyewe wakana. Warejeshwa rumande dhamana hadi Octoba 30. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, October 16, 2012

ALIYEKOJOLEA QUR-AAN APANDISHWA KIZIMBANI, Waliohisika na vurugu nao 37 wasomewa mashtaka wenyewe wakana. Warejeshwa rumande dhamana hadi Octoba 30.

Watuhumiwa wa vurugu za mbagala zilizo tokana na hasira za waisilamu waliopandisha jaziba baada ya mtoto wa miaka 14 kukojolea mkojo Qur-aani ijumaa iliyopita, wakirudishwa rumande baada ya kusomewa mashtaka kwenye mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam ambapo walikana mashitaka yote.


Watuhumiwa hao wakisubiri utaratibu wakuingia kwenye magari baada ya kusomewa mashtaka yao kwenye mahakama hiyo jana.

Miongoni mwa kina mama waliokamatwa na kudaiwa kuhusika na vurugu hizo wakishyka kwenye gari hilo walipofikishwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
MTOTO anaetuhumiwa kukojolea Qur-aani jana alipandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya kosa hilo sambamba na watuhumiwa wengine 37 waliohusika na vurugu baada ya tukio hilo.
Watu hao wameshtakiwa kwa mashtaka mbalimbali yakiwemo unyang'anyi wakutumia silaha,wizi pamoja na uharibifu wa mali mbalimbali zenye thamani vyenye thamani ya zaidi Shilingi 500Millioni ambazo ni zaidi ya dola laki tatu za kimarekani.
Mashtaka mengine waliosomewa na watuhumiwa hao kama walivyosomewa na upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Tumaini Kweka, ni paamoja na kuchoma makanisa kadhaa yakiwemoAnglikana, Lutheran, Sabato na Agape.
Kati ya washtakiwa hao 37 walikuwepo washitakiwa 17 walisomewa makosa ya ziada ambayo ni wizi wa kutumia silaha ambayo kwamujibu wa wa upande wa mashtaka makosa hayo hayana dhamana kisheria.
Kuhusu dhamana kwa washtakiwa makosa mengine ya wizi na uporaji hakimu anaesikiliza kesi hiyo amesema dhamana za watu hao zitakuwa wazi pale kesi hiyo itakapotajwa tena octoba 30 mwaka huu.
Na kuhusu Kesi ya mtoto aliyekojolea Qur-aan kesi yake inasikilizwa kwenye mahakama ya watoto na atapewa haki zote anazostahili kama mtoto kwenye usikilizwaji wa kesi hiyo na kwa sababu za kiusalamu tunalazimika kulihifadhi jina la mtoto huyo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here