Rais wa Kenya Mwai Kibaki akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Uganda Yowery Museven (kulia) wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya nchi hiyo.
UGANDA imeadhimisha
miaka hamsini ya uhuru wake huku wakuu kadhaa wa mataifa ya Afrika wakiungana
na Rais Yoweri Museveni katika sherehe hizo mjini Kampala. Wadadisi wanasema
kuwa Rais Museveni aliyeingia madarakani tangu mwaka 1986 ameiongoza nchi hiyo
kwa kudumisha amani na kuleta maenedeleo baada ya miaka mingi ya vita vya
wenyewe kwa wenyewe na unyanyasaji.
Lakini wakosoaji wake wanasema amekandamiza upinzani
nchini humo. Kiongozi wa upinzani Kizza Besigye aliyewekwa kizuizini mara mbili
wiki iliyopita anamshutumu Rais Museveni kwa kuiangamiza nchi hiyo iliyojipatia
uhuru wake toka kwa Waingereza.
Sherehe za leo zilihuduhuriwa na takriban viongozi 15 wa
Afrika wakiwemo marais wa miaka mingi, Robert Mugabe wa Zimbabwe na Yahya
Jammeh wa Gambia. Museveni hajasema ikiwa atawania urais katika uchaguzi mkuu
mwaka 2016, ingawa baadhi ya vigogo katika chama chake wanataka astaafu
wakisema kuwa anapoendelea kusalia mamlakani, ndivyo chama tawala kinaendelea
kupoteza ushawishi.
Kwa wanaharakati wa upinzani ,wasioona cha kusherehekea
wanasema kuwa Museveni amekua mamlakani nusu ya miaka ambayo nchi hiyo
imejitawala na hivyo wangetaka kutumia fursa hiii ya kusherehekea uhuru kumtaka
aondoke mamlakani.
|
No comments:
Post a Comment