KAMERA YA RAHA ZA PWANI IKIENDELEA KUPEKUA MWANZA. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, November 4, 2012

KAMERA YA RAHA ZA PWANI IKIENDELEA KUPEKUA MWANZA.

Hawa jamaa ninavyowafahamu ni wadau wa zuri wa mazingira na hisi hata hapa wanafanya kazihiyo ndio maana nirafiki wa binadamu hawabughudhiwi.
Hawa ndege kuna baadhi ya maeneo walikuwepo wengi lani wametoweka kutokana na binadamu kuwawinda na kuwadhuru lakini hapa wanalindwa vizuri sana ingawa kuna wengine wanaoneka na ulemavu wa miguu inaonekana kama walipigwa.
Mrundikano wa vyombo vya ziwani vilivyoharibika huchafua mandhari ya eneo la Mwaloni ambapo panapirika nyingi za kushusha na kupakia mizigo pamoja na biashara za aina mbalimbali unaleta mazingira ya uchafu na si taswira nzuri kwa jiji lenye sifa ya usafi wahusika waliangalie hili.
Hapo hapo Mwaloni kamera ya raha za pwani ikamulika mtoto huyu akijaza maji kwenye chupa kwenye chemba ya maji taka hata hivyo hakuweza kunieleza anayafanyia nini maji haya.

Taswira pekee ya shena ya kuni itakuonyesha namna misitu yetu inavyoteseka huko porini, bila kupata shida ukifika tu kwenye eneo la Mwaloni unapokewa na shehena hii ya kuni.

Soko lenyewe la mwaloni ni hili huku biashara kubwa kwenye eneo hilo ikiwa ni samaki na ndizi ingawa na biashara nyingine za aina mbalimbali zinafanyika.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here