Hawa ni warembo waliofanikiwa kufika kwenye tano bora kwenye fainali hizo za Misss Tanzania akiwemo na Brigit Alfred kushoto.
|
HATIMAE
uleutabiri uliofanywa na blog hii wa kubashiri
mrembo atakye chukua taji la Tanzania mwaka huu umetimia baada mrembo kutoka Kitongoji
Cha Sinza ambaye pia ni Miss Kinondoni Brigit Alfred kuibuka kidedea na kuwa Miss Tanzania kwenye shindano
lillomalizika hivi punde.
Ukumbi ulilipuka furaha mara baada ya
kutangazwa kwa mrembo huyo na kuhitimisha mchakato wa kumsaka mlimbwende wa
Tanzania.
Blog hii ilifanya uchambuzi kwa warembo wote 30 waliokuwa wakigombea taji hilo na kumbashria mshindi aliyenyakua ubingwa huo kuwa angeshinda kutokana na vigezo vya blog hii.
No comments:
Post a Comment