YALIYOJIRI BAADA YA LEMA KUSHINDA KESI. - RAHA ZA PWANI

Habari za Hivi Punde

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, December 21, 2012

YALIYOJIRI BAADA YA LEMA KUSHINDA KESI.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa Tiketi ya CHADEMA (aliekuwa amesimamishwa Ubunge),Mh. Godbless Lema akiwasalimia wanachamana na wafuasi wa Chama hicho waliokuwepo ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo.wakati alipofika kusikiliza Rufaa yake dhidi ya kesi ya Kupinga matokeo ya Uchaguzi dhidi yake iliyofunguliwa na Wanachana wa CCM jijini Arusha.Mh. Lema ameshinda Rufaa hiyo na kufanikiwa kurudishiwa nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo la Arusha mjini.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe (katikati) akiwa sambamba na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Godbless Lema (pili kulia) na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari wakiwa ndani ya Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusikiliza Rufaani ya kupinga matokeo ya Uchaguzi iliyokuwa ikimkabili Mbunge,Godbress leo ambaye ashinda Rufaa hiyo leo.
Wanachama na Wafuasi wa Chadema wakimshangilia Mbunge wao mara baada ya kushira Rufani ya kesi yake ya kupinga matokeo ya Uchaguzi jimbo la Arusha mjili iliyokuwa ikisikilizwa leo kwenye Mahakama ya Rufaa,jijini Dar es salaam.
 Wanachadema wakitembea kwa maandamano kuelekea kwenye ofisi za Chama chao zilizopo Kinondoni jijini Dar.
Mwanamama huyu ambaye ni Mama ntilie na hakutaka kuwa nyuma kishangilia ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mh. Godbress Lema.
 Pongezi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama,Mh. Wilbrod Slaa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here