MOTO uliowashwa na wananchi wa mkoa wa Mtwara kupinga gesi asilia kupelekwa Dar es
Salaam inazidi kuchochewa siku hadi siku baada ya juzi Mbatia kufanyiwa
vurugu, sasa msafara wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
unadaiwa kuzuiwa kwa magogo na mawe alipojaribu kutembelea kijiji cha Msimbati
ambako gesi asilia inavunwa.
Habari za kuaminika zilizolifikia blog hii
mjini Mtwara leo zinadai kuwa tukio hilo lilitokea saa 8 mchana mbapo waziri
huyo alilazimika kugeuza msafara wake katika kijiji cha Ziwani na kurejea mjini
Mtwara baada ya kutaarifiwa kuwa hali si shwari.
Habari zinadai kuwa waziri huyo aliwasili
mjini Mtwara kwa ndege ya asubuhi na kupokelewa na viongozi wa mkoa ambapo inadaiwa
kimyakimya alianza safari ya kwenda Msimbati kabla ya kupewa taarifa ya hali
tete ya usalama.
Mashuhuda wa tukio la kufungwa kwa barabara
wamesema kuwa baada ya wananchi kupata habari za ujio wa waziri huyo,
walionekana wazi kutokubalina, hivyo walijikusanya na kuamua kuifunga barabara
kwa kukata magogo na kuyalaza barabarani kwa lengo la kumzuia asiingie katika
kijiji hicho.
Gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari
ndiyo la kwanza kuwasili kwenye kizuizi hicho hata hivyo hawakudhuriwa zaidi ya
kuamriwa kugeuza gari na kuondoka.
Kubwa linalodaiwa kuwakasirisha wananchi
hao ni kauli za kejeli za viongozi wa serikali kuwa wananchi wa kijiji hicho
wananufaika na gesi asilia kwa kutumia umeme bure ili hali wanalipa ankara za
umeme kila mwezi.
“Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora George Mkuchika kupitia vyombo vya
habari wamesema sisi tunatumia umeme bure…hizi ni kejeli…ninazo bili za umeme
tangu nilipounganishiwa” alisema mkazi wakijiji hicho kwa sharti la kutotajwa
jina.
Aliongeza kuwa “Kana kwamba haitoshi leo
wanataka waje kututukana waziwazi ili wadhihirishe kuwa sisi ni wapuuzi,
hatujasoma …tumesema baasi, hatutaki kuonana na kiongozi yeyote yule”
Mwenyekiti wa kijiji cha Msimbati Salum
Athumani Tostao anathibitisha kuwapo kwa hali hiyo na kuongeza kuwa polisi
walikwenda kijijini hapo na kufyatua mabomu ya machozi kuwatisha wananchi hao
hata hivyo msimao wao uliendelea kuwa hawataki kuongea na waziri huyo.
“Walikuja polisi, kama kawaida yao
wakafyatua mabomu ya machozi hewani…hakuna mwananchi aliyekimbia, ilikuwa kama
mchezo wa mpira wa miguu wao wanafyatua mabomu hewani wananchi wanashangilia na
kuzidi kuongezeka eneo la tukio” alisema Tostao akiongea kwa simu.
Alifafanua kuwa “ Waziri hakuwahi kufika
huku, ilikuja gari moja iliyobeba waandishi, walipoona hali ni tete wakampigia
simu asije na ndipo polisi walipokuja badala yake…polisi waliacha kupiga mabomu
na
kuamua kuongea na wananchi ambao hawakuonesha
woga wowote, waliwaambia polisi hawataki waziri akanyaje ardhi ya kijiji chao”.
Alibainisha kuwa yeye kama kiongozi wa
kijiji hakupewa taarifa juu ya ujio huo na kwamba hilo halikumshangaza kwa
madai ni kawaida ya viongozi hao kuipuuza serikali yake kwa kuingia kijijini
hapo na kutoka bila ya kutoa taarifa kwake.
“Wananchi walipata taarifa kuwa waziri
au naibu wake anakuja na ndipo walipofunga barabara wakisema hawataki kumuona
akikanyaga ardhi yao…kwa bahati nzuri gari ya kwanz akufika ilikuwa ya
waandishi wa habari, kwa huruma wananchi wakawaambia warudi” alisema mwenyekiti
huyo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mary
Nzuki akiri wananchi kufunga barabara ingawa alikanusha madai ya Naibu Waziri
Simbachawene kuwapo ziarani mkoani hapa.
“Waandishi wa habari waliokwenda katika
ziara za kazi zao za kawaida ndiyo waliozuiliwa na wananchi hao…Naibu waziri
hajawahi kufika Mtwara kwa siku ya jana…wananchi walidhani hilo gari ni la
waziri lakini ukweli si yeye” alisema Kamanda Nzuki
Akizungumzia hilo Simbachawene alisema
“Hapana sio kweli, ningekuja hapo mjini singeweza kujificha…tatizo la wananchi
wetu hawajapata elimu sasa nitaendaje huko kimyakimya ili iweje….jana nilikuwa
ofisini na vikao kutwa nzima…nenda ‘airport’ (uwanja wa ndege) kaulize…hata mimi
nimeona kwenye jamii forum, ile ni ‘open paper’ (kurasa wazi) mtu yeyote
anaweza kuweka chochote”
Aliongeza kuwa “Inasikitisha, aheri wewe
uliyenipigia simu kuliko magazeti yanayochukua habari kwenye jamii
forum…inaonekana kuna watu wamedhamiria hili jambo hili”
Tukio hilo limetokea siku moja tangu
mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia afanyiwe vurugu na baadhi ya watu
katika mkutano wake wa adhara uliofanyika Uwanja wa Mashujaa mjini hapa na
badaye kutaka kumdhuru kwa madai ya kutoridhishwa na hotuba yake hali
iliyosababisha akatishe ziara yake.
Habari kwa Hisani ya Lindiyetu blog.
Leo 19 Jan 2013 kimenuka Mtwara,FFU na Mabomu mitaa ya Bima ,Exim na Tanesco ilikwa baada ya Tanesco kukata Umeme ambao ulikuwa unatumiwa na wananchi ktk mkutano wa wabunge wa mikoa ya Kusini mwa Tanzania wanaopinga bomba la Ges asilia kwenda Dar mpaka Serikali ijibu hoja za wakazi wa kusini kutokana na Lasilimali hiyo ,wanachi walivamia Ofisi ya Tanesco na kudai warejeshe umeme hapo ndiyo tafrani ilipoanza ,Huku mvua kubwa sana na mafuliko yakitawala mjini hapa,Wananchi wameazimia kupambana ilikudai haki zao,inasemekana wananchi wanampango kuwaodoa Askari wote wanaoishi kwa kupanga ktk majumba yao kwani ni wasaliti na wanawapiga,Gas kwanza uhai baadae.HAITOKI Gas Mtwara mpaka kieleweke
ReplyDelete