PROF.MAGHEMBE AKUTANA NA UJUMBE WA WIZARA YA MAJI YA MISRI, MTO NILE,ZIWA VICTORIA VYATAWALA MJADALA - RAHA ZA PWANI
Responsive Ads Here

Post Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 16, 2013

PROF.MAGHEMBE AKUTANA NA UJUMBE WA WIZARA YA MAJI YA MISRI, MTO NILE,ZIWA VICTORIA VYATAWALA MJADALA

Responsive Ads Here
DSC_0404
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na ujumbe wa watu wa Misri ulioongozwa na Waziri wa Maji wa nchi hiyo Dk.Mohamed Saad (kushoto) walipofika ofisini kwake kwaajili ya mazungumzo mbalimbali kuhusu sekta ya maji na umwagiliaji hassa suala la maji ya mto Nile ambayo chanzo chake ni ziwa Victoria. Magembe aliwataka kuimarisha Ushirikiano wa nchi hizo kwenye mambo yote wanayokubaliana na kwayale wasiokubaliana kuendelea na majadiliano.
DSC_0435
Waziri wa Maji wa nchini Misri Dk.Mohamed Saad (katikati) akizungumza kwenye mkutano na Waziri wa maji na Maofisa wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo, ambapo ujumbe huo wa Misri upo nchini pamoja na mambo mengine watajadili suala la maji ya Mto Nile ambayo Chanzo chake ni ziwa Victoria.
DSC_0431
Baadhi ya wajumbe walioshiriki mkutano huo kwenye Ofisi za Wizara ya Maji na Umwagiliaji jijini Dar es Salaam.
DSC_0427
Waziri wa Maji wa Misri  Mohamed Saad (katikati) akizungumza na watendaji wa Wizara ya Maji nchini kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Jumanne Maghembe kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Bilinith Mahenge.
DSC_0415
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania wakinukuu mambo mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa na ujumbe wa Wizara ya maji ya nchini Misri jijini Dar es Salaam leo.
DSC_0412
Balozi wa Misri nchini Tanzania Hossam Moharam (kushoto) akiwa sambamba ujumbe wa nchiyake uliofika nchini kwa majadiliano ya mambo mbalimbali ya sekta ya maji.
DSC_0410
Ujumbe wa Wizara ya Maji ya nchini Misri ukifuatilia majadiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad